The House of Favourite Newspapers

Maajabu ya Paka Mwizi wa Nguo za Ndani

0

Brigit (3)Nguo za ndani na soksi zilizoibwa na paka huyo anayeitwa Brigit

Hamilton, New Zealand

PAKA mmoja huko Hamilton nchini Uholanzi amegundulika kuwa na mchezo mchafu wa kuiba nguo za majirani na soksi hasa wakiwa wamelala usiku wa manane.

Brigit (1)

Taarifa zilizotolewa na mmiliki wa paka huyo, Sarah Nathan zimeeleza kuwa katika kipindi cha miezi miwili, paka huyo mwenye umri wa miaka sita ambaye anayejulikana kwa jina la Brigit aliiba nguo za ndani za ndani (boxer) 11 na zaidi ya soksi 50. Cha kushangaza ni kuwa, paka huyo huiba nguo za ndani za wanaume pekee.

Brigit (2)

Sarah Nathan aliandika ujumbe unaoelezea tabia ya paka huyo isiyo ya kawaida katika mtandao wake wa facebook na kueleza kushangazwa kwake na tabia hiyo huku akianika wazi namna ambavyo paka huyo amekuwa akimpa wakati mgumu hasa anaporudi nyumbani na vifurushi vya nguo alivyoiba huko mtaani.

Brigit (4)

”Tabia hiyo sasa inazidi kuwa mbaya. Lazima kuna mtu ambaye anakosa vitu vyake”, alisema katika ujumbe wake kwenye ukursa wa facebook lililosambazwa mara 500.

Brigit (6)Mmiliki wa paka huyo, Bi Nathan (kushoto).

Bi Nathan ameeleza kwamba tatizo la paka huyo kuwa mwizi lilianza alipogundua vipande kadhaa vya nguo za ndani katika nguo zake anapoziosha.

Brigit (7)Tangazo lililowekwa na Sarah Nathan kuhusu wizi wa paka huyo.

”Nguo hizo za ndani hazikuwa zetu, na siku moja Brigit aliingia katika chumba cha wageni (nyumbani kwa Nathan) akiwa amebeba soksi”, akisema kuwa waathiriwa wa Brigit walikuwa majirani katika nyumba za ghorofa.

Leave A Reply