The House of Favourite Newspapers

Maambukizi ya Corona Yafikia Milioni 1, Marekani Hali ni Mbaya

0

UGONJWA wa Covid-19 unaendelea kuathiri nchi mbalimbali duniani, huku maambukizi ya ugonjwa huo duniani kupitia virusi vya Corona yakifikia milioni moja, na watu wakiendelea kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Wakati huohuo Marekani inaendelea kuripoti visa vingi vya maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo vifo vya watu 1,169 vimeripotiwa ndani ya masaa 24.

Uchumi umeangamizwa na janga hilo, kama inavyoonyesha takwimu nyingine ambayo inatisha: katika wiki moja, Wamarekani milioni 6.6 wamepoteza kazi. Nusu ya watu duniani wamekwama kutokana na hatua ya kukaa nyumbani ambayo kwa baadhi ya nchi imekuwa yenye madhara makubwa.

Idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa ulimwenguni inazidi milioni moja leo Ijumaa, huku watu 52,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la AFP.

Ulaya ndiyo bara lililoathiriwa zaidi, lakini Marekani inaelekea kuwa kitovu kipya cha janga hilo, ikiripoti robo ya visa vya maambukizi. Idadi hii labda ni ndogo, kwa sababu ya ukosefu wa uchunguzi wa kutosha.

Nchini Marekani, idadi ya vifo katika masaa 24 imeiweka nchi hiyo kuwa na rekodi kubwa zaidi: vifo 1,169, kulingana na ripoti ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Johns Hopkins.

Leave A Reply