The House of Favourite Newspapers

MAAMBUKIZI YA UKIMWI YANAPUNGUA – TACAIDS

0
TUME ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Jumanne Issango, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
TUME ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS)
Mkutano ukiendelea na waandishi wa habari.

 

TUME ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS) imesema kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kinaendelea kupungua kutoka aslimia 0.32 kwa kipindi cha mwaka 2012 na kitafikia hadi 0.16 ifikapo mwaka 2018.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS , Jumanne Issango, amesema maambukizi ya virusi yanaendelea kupungua japokuwa kuna tofauti katika mikoa, wilaya na makundi maalum.

 

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya mwitikio wa kitaifa, Audrey Njelekela,   ameitaja mikoa inayoongoza kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kuwa ni pamoja na Njombe na Iringa ambapo mikoa iliyo chini kwa maambukizi ni Manyara ,Tanga na Lindi.

 

 

Aidha ameeleza kuwa TACAIDS inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na unyanyapaa wanaokutana nao waathirika wa ugonjwa wa ukimwi, upungufu wa raslimali-fedha baada ya wafadhili kuondoka na kuongezeka kwa watoto yatima.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

MAAMBUKIZI YA UKIMWI YANAPUNGUA – TACAIDS

Leave A Reply