Mabadiliko Katika Sheria za Uchaguzi Sasa Kuruhusu Wafungwa Chini ya Miezi 6 Kupiga Kura
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, amesema mabadiliko katika sheria za uchaguzi yameleta mabadiliko makubwa, na kwamba sasa wafungwa wenye kifungo kisichozidi miezi sita wanaruhusiwa kupiga kura wakiwa magerezani.
Makalla amesema wasimamizi wa uchaguzi badala ya kuwa viongozi watakua maafisa waandamizi wa umma, lakini mabadiliko yako mengi ni kwamba katika sheria hata wafungwa watapiga kura. Narudia kama mlikuwa hamjui, ndio mabadiliko ya sheria. Wafungwa ambao kifungo chao hakizidi miezi sita watapiga kura wakiwa magerezani. Hivo hivo kwa upande wa Zanzibar wanaiita vyuo vya mafunzo ndio magereza yenyewe na mahabusu.
Makalla ameyasema hayo siku ya Alhamisi Machi 06, 2025 wakati akizungumza na Wananchi pamoja na Viongozi wa CCM katika katika Mkutano wa ndani uliofanyika kwenye Uwanja wa Toto Tundu uliopo Segerea Ilala Dar es saam ikiwa