The House of Favourite Newspapers

Mabalozi, Wanachama CCM Wakumbushwa Umuhimu wa Kujitolea

0
KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Oganizaisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Issa Haji  Gavu akizungumza kwenye Kikao cha kawaida cha Balozi wa Shina na 4 katika Kata ya Ifunda, mkoani Iringa, ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Danniel Chongolo alikwenda kushiriki kikao cha shina hilo na kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Oganaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) issa Ussi Gavu amewaomba wanachama na mabalozi kuendelea kukumbushana umuhimu wa kujitolea kwa Chama hicho ili kiendelee kupata ridha ya kuongoza dola na kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu.

Ameyasema hay oleo Mei 29 ,2023 alipokuwa akizungumza kwenye Kikao cha kawaida cha Balozi wa Shina na 4 katika Kata ya Ifunda jimbo la Kalenga lililopo Iringa Vijijini baada ya Katibu Mkuu wa CCM ,Daniel Chongolo kushiriki kikao hicho, Gavu amesema kokote Duniani dhamira ya Chama cha siasa ni kushika dola.

“Na katika mfumo wa demokrasia huwezi kushika dola pasi na kuwa na wafuasi na wanachama wanakiunga mkono chama chako , kwa bahati nzuri tangia tuanze mfumo wa vyama vingi kwenye chaguzi zote tulizopita CCM imeendelea kupewa imani na wananchi wa Tanzania.

“Na kwa bahati nzuri Mkoa wenu wa Iringa haujawahi kushuka kwenye mikoa mitatu kwa ubora wa kikuchagua Chama Cha Mapinduzi , sasa tuendelee kuwepo na kwa mujibu wa Katiba yetu ya CCM inasema kila tutapokwenda kwenye uchaguzi kushinda ni wajibu wetu

“Kwa hiyo tukumbukushane kwenye umuhimu wa kuhudhuria vikao,tukihudhuria vikao vyetu tutakuwa tuko wanachama hai, hivyo hatuwezi kupoteza haki zetu na hatuwezi kukiona Chama chetu kinapoteza mvuto, wajibu , haki na umahiri wake kwa jamii tunayoingoza.”

Hivyo amewahimiza kulipia kadi zao, kushiriki vikao vinavyohusu ngazi zao kwani wakifanya hivyo watatimiza wajibu wao wa msingi na hivyo ndivyo wanavyoweza kukifanya Chama hicho kuendelea kuaminiwa, kuthaminiwa na kuendelea kuchaguliwa.

“Tumeona vyama vingine vipo vingi ndani ya nchi yetu lakini hakuna chama chenye muundo , muongozo na maelekezo unaokifikia chama chetu , tupo hapa kwenye ngazi ya shina hatukuja kwa kubahatisha, tumekuja kwa lengo la kukumbushana tunaamini kila mpiga kura kwenye nchi hii anakaa kwenye shina.

“Kwa hiyo ni wajibu wetu viongozi wa mashina , wajumbe wa mashina tuwachunge, tukuwambushe , tuwaelekeze , tuwanyooshe ili wananchi wanaokaa kwenye maeneo hayo waendelee kukipenda na kukiamini Chama Cha mapinduzi ili tuendelee kupata imani ya kuongoza nchi,”amesema.

Amesisitiza sababu ya kuongoza nchi kwa Chama chetu ziko nyingi lakini kubwa zaidi ni mioyo na udhati wa kutaka kuleta maendeleo kwa jamii wanayoingoza , kwa hiyo amewaomba mabalozi na wanachama kuendelea kukumbushana umuhimu wa kujitolea kwa Chama chao ili tuendelee kupata ridhaa ya kuongoza.

Leave A Reply