Kartra

Mabao Yampa Jeuri Kaseke Yanga

BAADA ya juzi Jumanne kufunga mabao mawili, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke, ameanza nyodo na kutamka hakuna nafasi aliyoipata ya wazi katika msimu huu na kukosa kufunga huku akiahidi kuendelea kutupia kila mchezo.

 

Kiungo huyo aliifungia Yanga mabao mawili kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui ukiwa ni mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam na kutinga nusu fainali ambapo watacheza dhidi ya Biashara United.

 

Nyota huyo ni kati ya wafungaji tegemeo hivi sasa katika kikosi cha Yanga ambaye kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, amefunga mabao sita.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaseke alisema: “Kwangu ninajisikia furaha, amenipa nafasi ya kuanza katika kikosi cha jana (juzi) tulipocheza dhidi ya Mwadui na kufanikiwa kufunga mabao mawili pekee ambayo yametupeleka nusu fainali.

 

“Binafsi ni kawaida yangu kufunga mabao na Wanayanga wafahamu kuwa sijabahatisha, ni uwezo wangu binafsi nilioutumia ambao ukatupa matokeo mazuri ya ushindi.”

STORI: WILBERT MOLANDI


Toa comment