Mabasi yanayojiendesha yenyewe kuanza kutoa huduma Marekani

61

Muonekano wa basi hilo dogo aina ya EZ10 likiwa barabarani.

3052100-inline-s-3-robot-buses-are-coming-to-a-san-francisco-suburb

….Yakiwa yamepaki.

easymile_0012

ligier-easymile-ez10

Abiria wakiwa ndani ya basi hilo.

MABASI yenye kujiendesha yenyewe, yataanza kutumika nchini Marekani hivi karibuni. Eneo la biashara la Bishop Ranch huko San Ramon, katika jimbo la California, litakuwa sehemu ya kwanza nchini humo kutumia mabasi yanayojiendesha yenyewe kwa mitambo maalum (robot) kusafirisha abiria.

Hatua hiyo itakuwa ni mwanzo wa utaalam wa kuendeleza magari yasiyokuwa na madereva kama yale yaliyoasisiwa na kampuni la Google ambapo mtihani mkubwa utakuwa ni kwa watu kuyazoea magari hayo.

Hii inatokana na ukweli kwamba njia za sasa na kasi ya chini ya maagari, havifanyizi mazingira mema kwa kuanzishwa kwa magari yasiyokuwa na madereva.

EZ10 ni basi lisilokuwa na dereva ambalo ni maalum kwa safari fupi. Gari hilo hivi sasa linafanya kazi barani Ulaya katika nchi za Finland na Ufaransa na hivi karibuni litaanza kazi nchini Hispania.

Magari hnayo ambayo hutumia umeme, hubeba abiria wanaofikia kumi na yana sehemu za kuwekea vigari vya kusukumwa vya walemavu (wheelchairs) na waenda kwa miguu ambao wanaweza wakapanda.

Magari hayo yamelenga kumfanya abiria ‘kuyadandia’ na kukufikisha mahali ambapo unakaribiakufika, na yamelengwa kwa kutumiwa katika sehemu za bustani za mapumziko.

Magari hayo ya EZ10 hutumia njia zilizopangwa na kuendeshwa kwa kutumia mitambo ya ‘laser’ ili kukwepa vitu vyovyote vilivyo katika njia yanayopita. Njia hii ni nyepesi zaidi kuliko ile inayotumiwa na magari ya Google ambayo ni lazima yakwepe au kupishana na magari mengine, waenda kwa miguu na vikwazo vyovyote vinavyoweza kujitokeza wakati yanapita kwa kasi katika barabara kuu.

Randell Iwasaki ambaye ni mkurugenzi wa kampuni la CCTA ambalo hufanya majaribio ya magari yasiyokuwa na madereva liitwalo GoMentum Station, anasema utaalam huu utawasaidia abiria kufika katika vituo vya kusafiria, maeneo ya biashara na kwenye sehemu mbalimbali za huduma na hivyo kukwepa adha ya kuendesha magari na kutafuta sehemu ya maegesho.

Loading...

Toa comment