The House of Favourite Newspapers

MABAWA APINGA MAANDAMANO YA KWENYE MITANDAO

Mwanaharakati, Laurence Jumanne Mabawa, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
...Akifafanua jambo.

 

MWANAHARAKATI  mzalendo ambaye alipata kuwa gumzo mwaka jana kwenye vyombo vya habari mbalimbali nchini, Laurence Jumanne Mabawa, amejitokeza na kupinga vikali harakati zinazoendeshwa na mitandao ya kijamii ya kuhamasisha maandamano.

 

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, mwanaharakati huyo awali aliyekuwa na kampeni ya ‘Magufuli Baki’ amesema kwamba ameamua kuja na kampeni nyingine aliyoipa jina la ‘Washa Data Tetea Taifa’ ili  kuweka sawa matumizi ya kimtandao yanayotumika vibaya nchini ambapo yasipodhibitiwa mapema na watu kupewa elimu ya matumizi mazuri ya mitandao hivyo,  kuna uwezekano kuleta athari mbaya kwa taifa letu.

 

Aidha mwanaharakati huyo alieleza kwamba ameamua kuja na kampeni hiyo ili kuwakumbusha vijana hasa wanaotumia vibaya mitandao hiyo waitumie vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa.

 

“Kwa sasa kumeibuka baadhi ya watu wasiolitakia mema taifa letu na amani tuliyonayo.  Watu hao wameanza maneno ya uchochezi  kupitia mitandao ya kijamii wakiwahamasisha Watanzania wachafue amani ya taifa letu kwa kuandamana, jambo ambalo halikubaliki na linalotakiwa lilaaniwe na kila mpenda amani,” aliseme.

 

Aliongeza kwamba haiwezekani kuhamasisha maandamano ya uvunjifu wa amani kwenye nchi ambayo viongozi wake wanawajibika ipasavyo kwa kuwatumikia wananchi wake.

 

Amemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumuunga mkono  hasa siku ya Aprili 26 ambayo ni siku ya Muungano,  iweze kutolewa elimu  ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii  ili kila Mtanzania aweze kuelewa matumizi bora ya mitandao.

 

Comments are closed.