The House of Favourite Newspapers

Mabeste Aanika ‘Yaliyomo’ Kwenye Ndoa Yake

Mabetse na Mkewe, Lisa Fickensche,

MWANAMUZIKI anayefahamika zaidi kwa jina la Mabeste, ambaye hivi karibuni aliachia Wimbo wa Sijui, amefunguka mengi muziki wake na chang-amoto zilizokuwa zinamkabili kwenye ndoa yake kutokana na muziki huo.

 

Akipiga stori na Risasi Vibes, Mabeste alisema amepitia mengi kwenye muziki lakini hawezi kuacha japokuwa ameamua kutafuta kazi nyingine ya kufanya ili kutanua wigo wa kujiingizia kipato. “Unajua kwa sasa wanamuziki wamekuwa wengi sana na changamoto zimeongezeka tofauti na ilivyokuwa mwanzo kipindi ambacho wanamuziki walikuwa wachache.

 

“Sasa kwa wengine ambao tunaweza kuendelea na mambo mengine imebidi kujiweka kando kidogo huku tunafanya muziki lakini pia tunaendelea na maisha mengine, kwa sababu muziki ni kama zilivyo biashara nyingine,” alifunguka Mabeste.

 

Kuhusu hali ya mkewe, Lisa Fickensche, aliyekuwa anasumbuliwa na matatizo ya moyo kwa muda mrefu, Mabeste alisema kwa sasa yupo vizuri.

 

“Kuhusu changamoto kwenye ndoa zilikuwepo wakati nimeingia na zilipokuwa zikitokea nilikuwa sijui kuzitatua kama mwanandoa, bali nilikuwa nachukulia mimi ni mtu maarufu na mwanamuziki, kwa hiyo nilihitaji kuwa juu ya kila kitu.“Lakini baadaye nilikuja kuelewa kwamba nakosea na kujirekebisha,” alisema Mabeste.

Boniphace Ngumije.

Comments are closed.