The House of Favourite Newspapers

MABESTE AWAPONDA WANAODHALILISHA WANAWAKE

Venance William ‘Mabeste’

MKALI wa Muz-iki wa Hip Hop Bongo aliyekuwa anafanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Venance William ‘Mabeste’ amechukizwa na watu wasiowa-thamini wanawake ambao wako nao kwenye kwenye uhusiano.  

 

Mabeste alisema hayo baada ya kuwepo matukio mengi ya wavulana kudhalilisha wanawake waliozaa nao au waliokuwa nao likiwemo lile la muigizaji Wema Sepetu na mpenzi wake PCK.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Mabeste alisema kuwa, vijana inabidi wajitambue na kuwaheshimu wake zao kama ambavyo wanawapenda na kuwaheshimu mama zao kwa sababu wanastahili heshima na thamani.

 

“Unapomdhalilisha mke wako au mwanamke wako ni sawa na umejidhalilisha mwenyewe kwa sababu mwisho wa siku nyie ni mwili mmoja, kama mnafikia uamuzi wa kuachana achaneni kwa amani sio mpaka kila mtu ajue majirani au mitandaoni,” alisema Mabeste.

STORI: SHAMUMA

Comments are closed.