Mabeste Aitambulisha Back Off Global Radio – Video

RAPA mkali Bongo, Mabeste amefanya ziara katika kampuni ya Global Group na kutambulisha mkwaju wake mpya, Back Off, kupitia spika za +255 Global Radio, kwenye kipindi cha Bongo 255 kinachosimamiwa na Stewart George pamoja na Lady T.

 

Mabeste ametoa mkwaju huo baada ya ngoma yake ya Qualify aliyoitoa Januri 10 kufanya poa na kumrudisha kwenye chati ya muziki ambayo aliikosekana kwa kipidi kirefu kidogo.

Akitambulisha ngoma hiyo Mabeste alisema, alipata wazo la kuandika wimbo huo kutokana na maisha ambayo aliyapitia kipindi cha nyuma ikiwemo kusalitiwa na kuachana na mke wake Lissa, huku akiongeza kuwa mashairi mengine kwenye wimbo huo yametokana na kuona maisha ya watu wengine wa mtaani.

 

“Siwezi kuandika kitu ambacho kipo nje na maisha ambayo ninayaishi, Back Off ilitokana na maisha ambayo nilipitia hapa katikati, kwahiyo niliposikia huu mdundo wakati nipo studio, niliona kabisa unahitaji kitu kama stori fulani ndiyo maana nikaandika,” alisema Mabeste.

 

Kuhusu ishu ya kuachana na mke wake, Mabeste alisema kuwa kwa sas ana mahusiano mengine kama ilivyo kwa mzazi mwenzake huyo, ingawa alikiri bado anampenda kwa kuwa ni mwanamke ambaye alimuoa na kuanzisha naye familia.

“Nina mahusiano mengine kwa sasa, lakini sitaki yawe wazi tu, ikitokea labda ni bahati mbaya. Lissa bado nampenda kama mwanamke ambaye nilimuoa na kuanzisha naye familia kwahiyo tutabaki kuwa kama familia milele na ninatamkia kila la kheri kwenye mahusiano yake ya sasa,” alisema Mabeste.

 

 

Mabeste alitumia nafasi hiyo pia kuwashukuru mashabiki kwa kuendelea kusapoti mziki wake na kumfanya aendelee kufanya mziki licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali na kwa sasa yupo kwenye mejimenti mpya ya Dole Entertainment.

“Nawashukuru mashabiki wangu kwa kuipokea Qualify ba kuifanya iwe nyimbo kubwa, naomba na hii pia waipokee na iwe kubwa kuliko kazi zingine ambazo ziliwahi kutoka hapo nyuma, wamekuwa nami katika magumu na mazuri hivyo waendelee kunishika mkono,” aliongeza Mabaste.


Loading...

Toa comment