visa

Mabilionea Wasio na Huruma 44

WAKATI Dk Viola na nduguye Vanessa wamejificha nchini Tanzania wakiwa katika sura mpya za wazee wa Kijapan na wamekaribishwa katika nchi hii ambayo ni asili yao kama wawekezaji waliopewa Kisiwa cha Bongoyo ili wajenge mji wa kisasa, mpelelezi Inspekta Masala bado yupo nchini Thailand akiendelea kuwatafuta wanawake hao hatari.

Jambo baya linamtokea Inspekta Masala, wapelelezi wote aliokuwa nao wameuawa kwa mtindo mmoja wa sindano ya heroine na chupa ya Vodka ili kuonekana kama vile walizidisha dawa na kunywa pombe nyingi, jambo ambalo yeye haliamini kwani watu wake hawakuwa watumiaji wa dawa za kulevya,  anachojua ni kwamba, Dk Viola na nduguye Vanessa ndiyo wanaofanya mauaji hayo.

Je, nini kitaendelea leo?  Atauawa pia? Au atawakamata wanawake hawa hatari? 

 SONGA NAYO…

HAPAKUWA na kificho tena, kila kitu kilikuwa wazi kwamba kuna mtu alikuwa akiwaua wapelelezi wote waliotumwa na CIA, Scotland Yard na Interpol kuwasaka Dk Viola na Vanessa nchini Thailand, vifo vya Dennis Clapton na Celine Amber vilithibitisha jambo hilo, Inspekta Masala hakuwa na mashaka tena moyoni mwake kwamba sasa aliyetakiwa kufa ili kazi ya kuua wapelelezi ikamilike alikuwa ni yeye.

Hofu ikamuingia, kwa mara ya kwanza akajisikia kutetemeka, alikuwa amegundua watu aliokuwa akiwachunguza walikuwa ni hatari kuliko Kundi la Mafia, kila alipofikiria kwamba walikuwa ni wanawake alishindwa kuamini kama duniani kulikuwa na wanawake hatari kiasi hicho.

“Haiwezekani, hapa lazima kuna mkono wa wanaume, wanawake?  Waue kwa mtindo wa aina hii tena bila kugundulika na waondoke salama, haiwezekani, ila kwa mimi watakuwa na kazi ngumu sana kunitoa uhai, labda waje na mbinu nyingine!” Inspekta Masala alijifariji akiigusa bastola kiunoni kwake.

Bastola yake ilikuwa ni Revolver 249, bunduki ya kisasa iliyotengenezwa Uingereza yenye uwezo wa kubeba risasi ishirini na nne, kwenye mfuko wa koti lake Inspekta Masala alikuwa na magazini nyingine tatu zilizojaa risasi, kufanya awe na jumla ya risasi tisini na sita, lakini bado alikuwa na hofu, vifo vya wapelelezi wake vilimtisha na picha iliyomjia kichwani mwake ilikuwa ni ya kifo.

“What do I do now?” (Ninafanya nini sasa?) alijiuliza kichwani mwake baada ya kugundua kulikuwa na maiti mbili alizotakiwa kuzishughulikia ili zisafirishwe kwenda nchini Uingereza, akafikia uamuzi wa kupiga simu makao makuu ya Scotland Yard kuwapa taarifa juu ya kilichotokea.

“They killed them!” (Wamewaua)

“How?” (Wamewauaje?)

“The same style, a heroine injection in the vein, with a Vodka bottle on the side!” (Kwa mtindo uleule, sindano ya dawa ya kulevya aina ya heroine kwenye mshipa na chupa ya Vodka pembeni!”

“Oh, my God, were they drug addicts?” (Mungu wangu, walikuwa wateja wa madawa?)

“Of course not, it is just a killing style these women use!” (Hawakuwa wateja, huu ni mtindo tu wa kuua ambao hawa wanawake wanautumia!)

“These women are dangerous!  But where are they?” (Hawa wanawake ni hatari!  Wako wapi lakini?) aliuliza Mkurugenzi wa Scotland Yard.

“That question is killing me, I have never had a difficult case like this, I know they are here in Thailand but I have no idea where, I have turned the country upside down and shook it, but they are nowhere to be seen!” (Hilo swali linaniua, sijawahi kuwa na kesi ngumu kiasi hiki, najua wako hapa Thailand lakini sijui ni wapi, nimeigeuza Thailand chini juu na kuikung’uta lakini hawaonekani!) alimalizia Inspekta Masala mwili ukitetemeka.

“Are you okay?” (Uko sawa?)

“No!  I am in great danger, it seems I am the next target!” (Hapana!  Nipo katika hatari kubwa, inaonekana mimi ndiye ninayefuatia kufa!)

“Take care of yourself, we are doing arrangements for the bodies to be shipped to England as soon as possible!” (Jichunge sana, tunafanya kila kinachowezekana ili miili isafirishwe kuja hapa Uingereza haraka iwezekanavyo).

“I will!” (Nitafanya hivyo!)

Siku tatu baadaye miili ilipoondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Suvarnabhumi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Thailand, Shirika la Upelelezi la Thailand liitwalo Central Investigation Bureau of Thailand lilitoa taarifa kuwa wauaji wa Dennis na Celine waliingia hotelini hapo wakiwa wamevaa sare za wafanya usafi vyumbani na kufanya mauaji hayo kisha kuondoka bila kugundulika, ripoti hiyo ilizidisha hofu ya Inspekta Masala kupita kiasi.

Uamuzi aliofikia kwanza ni kurejea tena kwenye hospitali ambayo Dk Viola na Vanessa walifanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura, bado alihitaji kukutana na Dk Jeremy ili angalau aweze kumwelezea vizuri juu ya sura ambazo wateja wake walikuwa nazo baada ya upasuaji, hizo ndizo zingefanya kazi ya kuwakamata iwe rahisi, bila hivyo hata kama angekutana nao njiani angewaona ni watu wema kumbe ndiyo wauaji wake.

“I have to go back and talk to the doctor!” (Inabidi nirejee nikaongee na daktari!) aliwaza Inspekta Masala akiwa chumbani baada ya kutoka uwanja wa ndege, maongezi na Dk Jeremy, daktari bingwa wa upasuaji maarufu kuliko wengine wote nchini Thailand na bara zima la Asia yalikuwa ni ya muhimu mno ingawa hakuwa na uhakika kama angepata ushirikiano wa kutosha.

Baada ya kusitasita kwa muda akikumbuka mazungumzo ya mwisho na daktari huyo, hatimaye aliamua kuchukua hatua ya kuwasha gari na kwenda hadi kwenye hospitali yake, umbali wa kama dakika ishirini na tano hivi kwa gari kutoka hoteli aliyofikia. Kabla hajaifikia hospitali alishangazwa na umati mkubwa wa magari uliokuwa umeegeshwa mbele ya jengo, moyo ukashtuka.

“What’s happening here?” (Nini kinaendelea hapa?) alimuuliza mwanamke mmoja baada ya kuegesha gari lake na kushuka.

“Haven’t you heard?” (Hujasikia?)

“Yes, I haven’t!” (Ndiyo sijasikia!)

“Doctor Jeremy passed away a day before yesterday, today is his funeral” (Dk Jeremy alifariki juzi, leo ni mazishi yake!)

“Oh, my God!” (Mungu wangu!) alisema Inspekta Masala akijishika mikono kichwani.

“Sorry, are you his friend?” (Pole, wewe ni rafiki yake?)

“Yes!” (Ndiyo).

“He was a good doctor, but he died a bad death!” (Alikuwa daktari mzuri lakini amekufa kifo kibaya!)

“How did he die?” (Alikufaje?)

“We didn’t know he was a drug addict under heroine, he overdosed himself and drunk a bottle of Vodka!” (Hatukujua alikuwa mteja wa unga akitumia heroine, alijichoma dozi kubwa na kunywa chupa ya Vodka!)

Kauli hiyo iliwasha taa nyekundu kichwani mwa Inspekta Masala, akaelewa mara moja kilichotokea, aliyewaua wapelelezi wake ndiye aliyemuua Dk Jeremy ili kupoteza ushahidi kabisa wa kwamba waliwahi kubadilishwa sura.  Machozi yakamtoka Inspekta Masala, kifo cha Dk Jeremy kikawa kimeongeza maumivu na hofu moyoni mwake, hakika aliyetakiwa kufa baada ya hapo ni yeye peke yake.

Akamvuta mwanamke huyo pembeni ili apate kumdadisi zaidi, katika mazungumzo yao aligundua kuwa mtu aliyekuwa akizungumza naye alizaliwa mwanaume, Dk Jeremy akamfanyia upasuaji wa kumbadilisha jinsia na kumfanya awe mwanamke kabisa kiasi cha mtu kushindwa kumtofautisha na wanawake.  Jikedume huyo aliongea kwa uchungu mno akisimulia jinsi Dk Jeremy alivyokuwa mtu mwema.

“So you are a transgender?” (Kwa hiyo umebadilishwa jinsia?)

“Yeah!  I was born a boy, my name was Jensen but now I call myself Jen!” (Ndiyo!  Nilizaliwa mvulana, jina langu lilikuwa Jensen lakini sasa najiita Jen!) aliongea kijana huyo aliyekuwa amevalia wigi la rangi ya dhahabu, nyusi zake zikiwa zimetindwa vizuri, kwa kumuangalia alitaka kujifananisha na mwanamuziki wa Kimarekani, Britney Spears, hakika alikuwa mzuri, hata Inspekta Masala mwenyewe moyoni mwake alikiri kwamba hakutakiwa kuwa mwanaume.

“When was your operation performed?” (Upasuaji wako ulifanyika lini?)

“Four years ago!” (Miaka minne iliyopita).

“Oh!  Four years ago!  So you must be aware of the scene when CIA dropped on the roof of this hospital from a helicopter!” (Oh!  Miaka minne iliyopita, kwa hiyo lazima utakuwa unakumbuka tukio la CIA kutua kwenye paa la hospitali hii kutoka kwenye helikopta!)

“Yeah!  I was here that day!” (Ndiyo!  Nilikuwa hapa siku hiyo!)

“What?” (Nini?)

“I was here that day, admitted in room number three!” (Nilikuwa hapa siku hiyo, nimelazwa kwenye chumba namba tatu!)

“You must be kidding!” (Lazima unatania!)

“Why?” (Kwa nini?)

“Do you know two women who came here for face change?” (Unawajua wanawake wawili waliokuwa hapa siku hiyo kwa kubadilishwa sura?)

“Yes!  We were admitted in the same room, they left a few minutes before the CIA came!” (Ndiyo! Tulikuwa tumelazwa chumba kimoja, waliondoka dakika chache kabla CIA hawajafika!)

“Do you know how they looked after the operation?” (Unajua walifananaje baada ya upasuaji?)

“Yes, I took pictures with them before and after the operation!” (Ndiyo, nilipiga nao picha kabla na baada ya upasuaji!)

“What?” (Nini?)

“Yes, why are you shocked?” (Ndiyo, kwa nini umeshtuka?)

“Do you have the photos?” (Unazo picha?)

JE, nini kitaendelea?  Fuatilia siku ya Jumatatu katika Gazeti la Championi Jumatatu.
Toa comment