The House of Favourite Newspapers

Mabilionea Wasio na Huruma 40

0

OB-WK036_Dollar_G_20130219073815DK Viola na pacha wake Vanessa wamefanikiwa kufika nchini Thailand salama kabisa na sasa wapo katika Hospitali ya Thailand Cosmetic and Plastic Surgery Center kwa ajili ya kufanya upasuaji ili kubadili sura zao, wakiamini kabisa kwamba baada ya kufanya upasuaji huo, basi maisha kwao yangekuwa raha mustarehe.

Upande wa pili wa hadithi hii, tunawaona wapelelezi wa CIA, Interpol na Scotland Yard, wakiongozwa na mpelelezi mashuhuri Inspekta Masala, wanafuatilia nyendo zote za Dk Viola na nduguye, mwisho wanagundua kwamba waliingia katika kituo cha Thailand Cosmetic and Plastic Surgery Center, ni hapo ndipo wanapofikia uamuzi wa kutumia helikopta wakiamini kuwapata wahalifu hao na kuwatia kwenye mkono wa sheria. Je, watafanikiwa kuwapata Viola na Vanessa? Nini kinaendelea? SONGA NAYO…

WAPELELEZI wa Scotland Yard, CIA na Interpol wakiongozwa na Inspekta Masala, walitua juu ya jengo la Hospitali ya Thailand Cosmetic and Plastic Surgery Center na helikopta ikaondoka zake, kishindo kikasikika juu ya jengo hilo la ghorofa mbili na kusababisha watu wote waliokuwemo ndani kupatwa na mshtuko, kazi ya wapelelezi hao haikuwa nyingine, isipokuwa moja tu; KUWAKAMATA WAUAJI DK. VIOLA NA PACHA WAKE VANESSA, waliokuwa wakihitajika kwa gharama yoyote ile kutokana na matendo ya kinyama waliyoyafanya.

Magari mengine mawili yaliyojaza askari zaidi ya kumi wenye silaha, yalikuwa njiani huku yakipiga king’ora na kupishwa na magari mengine yaliyokuwa barabarani, madereva walitaka wafike eneo la tukio haraka ili kuongeza nguvu kama kungekuwa na ugumu wowote katika kazi ya kuwatia nguvuni Dk Viola na Vanessa walioaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia silaha.

Dk Jeremy Ho akiwa katikati ya upasuaji wa mwanaume aliyekuwa akibadilisha jinsia yake ili awe mwanamke, alisikia kelele ndani ya hospitali, mikono yake ikafa ganzi kwa hofu, hakuwahi kujisikia hivyo kabla. Kabla hajafanya lolote, mlango wa chumba cha upasuaji ulifunguka kwa nguvu, wakaingia watu wawili wenye bunduki.

“Who are you?”(Ninyi ni akina nani?)
“CIA, Interpol and Scotland Yard!”
“I don’t care what kind of a crap you are, get out of the operation theatre! How can you enter this room without wearing gowns and scrubbing your hands? Don’t you know you can cause infection to my patient, get out!”(Sijali ninyi ni takataka za aina gani, tokeni chumba cha upasuaji! Mnawezaje kuingia chumba hiki bila kusugua mikono yenu na kuvaa mavazi ya upasuaji? Tokeni nje!) alifoka Dk Jeremy Ho akimaliza kushona sehemu za siri za mgonjwa wake aliyekuwa katikati ya usingizi sababu ya dawa ya nusu kaputi.

“Sorry Doctor, we just want to know if you have patients by the names of Jackline Martin and Fionna Jones!”(Samahani daktari, tunataka tu kufahamu kama una wagonjwa wanaotumia majina ya Jackline Martin na Fionna!)

“Are you okay mentally?”(Una akili sawasawa?) badala ya kujibu swali, Dk Jeremy Ho alimuuliza muuliza swali, huku akiendelea na kazi yake ya kuunganisha mwili kwa nyuzi.
“Yes!”(ndiyo!)
“Then get out, wait for me at reception!”(Basi toka nje, nisubiri mapokezi!)
“We can’t wait!”(Hatuwezi kusubiri!)
“Then I can’t answer your questions!”(Basi siwezi kujibu maswali yenu!)

Inspekta Masala alibaki akishangaa, katika maisha yake ya kufanya kazi za upelelezi, hakuwahi kukutana hata mara moja na binadamu ambaye hakuogopa askari kama aliyekuwa mbele yake, ilibidi atabasamu, mwisho akawaamuru wenzake wamfuate badala ya kuendelea kupoteza wakati chumba cha upasuaji!

Walichokifanya ni kuvamia kila chumba ndani ya jengo hilo wakiwatafuta Dk Viola na Vanessa, kazi ambayo haikuwa na mafanikio baada ya kupekua kila mahali mpaka uvunguni mwa kila kitanda. Wakati wanamalizia ndipo Dk. Ho alijitokeza kutoka chumba cha upasuaji na kuwaomba wamfuate ofisini wake.

“How can I help you?”(Niwasaidieje?)
“We are looking for Jackline Martin and Fionna Jones!” (Tunawatafuta Jackline Martin na Fionna Jones)

“They are not here, I discharge them at 12:00!”(Hawako hapa, niliwaruhusu saa sita kamili!)
“They came here for?”(Walikuja hapa kufanya nini?)
“This is a hospital, people who come here have problems!”(Hii ni hospitali, watu ambao huja hapa wana matatizo!)

“Can we know what were their problems?”(Tunaweza kujua tatizo lao lilikuwa nini?)
“It is unethical for me to reveal my patients conditions without their consent!” (Ni kinyume cha maadili kwangu mimi kuzungumzia hali ya wagonjwa wangu bila ruhusa yao!)
“But this is important!”(Lakini hii ni muhimu!)
“My profession is more important!” (Taaluma yangu ni muhimu zaidi!)

Walijaribu kwa uwezo wao wote kumshawishi awaeleze kitu kilichofanyika na kama walibadilisha sura walikuwa katika muonekano gani lakini Dk Ho aliendelea kugoma, mwisho kwa sababu walipishana nao kwa dakika chache tu kabla hawajaondoka, walijua hawakuwa mbali sana na eneo hilo, lazima walikuwa bado wapo ndani ya Jiji la Bangkok na ilikuwa rahisi zaidi kuwakamata kabla hawajatoroka kwenda nchi nyingine.

“Let’s leave this stiff doctor alone, we are wasting time, we have to arrest them before they get out of Bangkok!”(Hebu tumuacheni huyu daktari mwenye misimamo, tunapoteza muda, lazima tuwakamate kabla hawajaondoka Bangkok!) alisema Inspekta Masala baada ya askari waliokuja na magari kuwasili.

Haraka wote wakatoka nje na kuingia ndani ya magari huku Inspekta Masala akiwasiliana na Jeshi la Polisi la Bangkok ili kuwekwe vizuizi kila mahali na upekuzi mkali ufanyike kwenye viwanja vya ndege kuhakikisha kwamba Dk Viola na Vanessa hawaondoki nchini Thailand kwenda mahali kwingine kokote duniani.

“There is no escape for them!” (Hakuna jinsi ya wao kutoroka!)
“For sure!” (Hakika!)
Waliongea wakiwa ndani ya gari kuelekea mjini, wakashangazwa na idadi ya vizuizi walivyokutana navyo njiani na kuuliza kama Dk Viola na Vanessa walipita maeneo hayo, jibu walilokutana nalo ni “HAPANA” kwani hata wapekuzi kwenye vizuizi hawakuelewa sura za watu waliokuwa wakiwatafuta, hiyo ndiyo ilifanya kazi ya kuwakamata iwe ngumu kupindukia.

“We will finally arrest them!”(Mwisho tutawakamata tu!)

Kazi hiyo iliendelea kila siku kwa mwezi mzima bila Dk Viola wala Vanessa kukamatwa, Inspekta Masala alichanganyikiwa kabisa, hakuwahi kukutana na wanawake wajanja kiasi hicho maishani mwake. Bado aliamini walikuwepo Bangkok, lakini hakujua ni sehemu gani waliyojificha, alishapekua kila kificho na kila hoteli lakini hawakupatikana.

Televisheni na vyombo vyote vya habari vilikuwa vikitangaza juu ya watu hao na zawadi nono ya dola milioni tano ilikuwa imetolewa na kuwafanya wananchi masikini wa Thailand kila siku wawe barabarani kuwasaka Dk Viola na Vanessa kwa majina yao ya John Hui na Lin Chu wakitumia sura zao za zamani. Jambo ambalo hawakulielewa ni kwamba wanawake hao wawili walikuwa ni wazee wawili wenye umri mkubwa na ndevu nyingi.

***
Waziri wa Utalii na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jamhuri Azimio na Katibu Mkuu wake, Teofil Ezekia pamoja na viongozi mbalimbali wa Bodi ya Utalii na Uwekezaji, walikuwepo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kupokea wawekezaji wawili raia wa Thailand ambao waliishi na kufanya biashara zao nchini Dubai.

Walikuwa wakija nchini kukubaliana na serikali ili wakinunue Kisiwa cha Bongoyo ili wakibadilishe kabisa na kukifanya mji mpya wa kitalii, wenye kila kitu kuanzia mahoteli, burudani na fukwe nzuri. Kwa kauli yao walitaka kukifananisha kisiwa hicho na Hong Kong.

“Watasaidia sana kukua kwa uchumi wetu!”
“Kabisa mheshimiwa.”
“Wawekezaji wa aina hii ndiyo tunaowahitaji.”
“Hakika.”
“Watalipa kodi ambayo itasaidia kuboresha maisha ya watu wetu!”
“Ni jambo jema.”

“Tusiwasumbue kabisa kwenye mchakato wa kusajili kampuni kama tutakubaliana nao kununua hicho kisiwa, wanatoa kiasi kikubwa mno cha fedha kupata asilimia sabini ya hisa!”
“Kwani wanalipa kiasi gani mheshimiwa?” Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii bwana Ramadhan Semvua aliuliza.

“Dola milioni mia moja na arobaini.”
“Aah! Ni fedha nyingi.”
“Ndiyo maana si vyema kusumbua wawekezaji wa aina hii wakati rais wetu anazunguka huku na kule duniani kutafuta wawekezaji, halafu wakija hapa nyumbani tunawasumbua.”

“Hatutafanya hivyo kabisa, nitahakikisha kila kitu kinakwenda sawa!” Katibu Mkuu alimalizia mazungumzo hayo kabla wote hawajanyanyuka kwenda kwenye ndege kuwapokea bwana John Hui na Lin Chu baada ya ndege kutua.

Zuria jekundu lilikuwa limetandikwa ardhini kwa ajili ya kuwapokea matajiri hao ambao waliposhuka walikumbatiana na waziri ambaye alianza kuwatambulisha kwa watu wote aliofika nao uwanjani, kisha kuelekea moja kwa moja kwenye jengo la watu maarufu ambako walisaini vitabu vya wageni na kutoka uwanjani hadi nje ambako waliingia kwenye gari, safari ya kuelekea Ikulu ya Magogoni ambako walitakiwa kula chakula cha mchana na Rais ilianza.

“Hakyanani tena, nimeimiss Bongo!” bwana Lin Chu alimnong’oneza John Hui masikioni kwa sauti ya chini kabisa bila mtu yeyote kusikia.

Safari ikaendelea kwa kasi, mbele kukiwa na askari wa pikipiki ili kufanya msafara usikwame mahali popote, mheshimiwa waziri ndiye alikaa kiti cha mbele akionekana mwenye furaha nyingi kwa ushindi wa kupata wawekezaji.

“Is it your first time in Tanzania?”(Hii ni mara ya kwanza ninyi kuwa Tanzania?)
“Yeah!”(ndiyo!)
“How do you see our country?” (Mnaionaje nchi yetu?)
“Ooh! Very beautiful!”(Ooh! Nzuri sana!) waliongea wote kwa pamoja kwa sauti ya kukwaruza.
“Do you have flu?(Mna mafua?)

“No! Why?”(Hapana! Kwa nini unauliza?)
“Your voices!”(Sauti zenu!)

JE, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Ijumaa katika Gazeti la Championi Iju

Leave A Reply