The House of Favourite Newspapers

Mabingwa wa Ligi Yanga kuweka kambi Ulaya Maandalizi ya msimu wa 2024/25

0

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa mpango mkubwa ni kuweka kambi Ulaya ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2024/25. Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24 walitwaa taji hilo baada ya kufikisha pointi 71 na walimaliza msimu wakiwa na pointi 80 kibindoni.

Leo Juni 15 2024 wanatarajia kufanya uzinduzi wa kitabu cha historia ambacho kitakusanya matukio yote muhimu yaliyopita ndani ya miaka 89 ya timu hiyo.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwa msimu ujao ni kufanya vizuri zaidi na wanatarajia kuweka kambi Ulaya huku kukiwa na mialiko kutoka nchi nyingine ambazo zinahitaji kuona timu hiyo inakwenda kucheza mechi za kirafiki.

“Kuelekea maandalizi ya msimu mpya tunatarajia kwenda Ulaya na kumekuwa na mialiko kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Kenya kote huko nah ii inatokana na ukubwa wa timu.”

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, GPL

BOIMANDA wa BODI ya LIGI – ”TUZO ni za WACHEZAJI BORA SIYO TUZO za WATANZANIA – UNAONEKANA MBAYA”

Leave A Reply