The House of Favourite Newspapers

Mabinti wa Chibok Waliotekwa na Boko Haram Wagoma Kurudi Nyumbani

Kundi la Boko Haram limetoa video mpya ikionyesha wasichana 14 waliotekwa katika mji wa Chibok, Kaskazini mwa Nigeria mnamo mwezi Aprili 2014 ambapo katika video hiyo wamesema kamwe hawatarejea nyumbani kwa sababu sehemu wanayoishi sasa ni takatifu na wanapata kila wanachohitaji.

 

Mabinti 300 wa Shule ya Chibok walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram mwaka 2014 ambapo baadhi yao walifanikiwa kutoroka licha ya wenzao kubaki na hawajulikani walipo. Kumekuwa na picha na video ambazo Boko Haram huzitoa mara chache ili kuwaumiza wazazi wao.

Kundi hilo limekuwa maarufu katika ukanda wa Afrika Magharibi kufanya vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya kinyama miongoni mwa raia. Inasemekana mabinti hao wanawatumikisha kingono.

Comments are closed.