The House of Favourite Newspapers

Mabinti Zaidi ya 3000 Wawezeshwa Program ya Kompyuta, Code Like A Girl

Dar es Salaam, 7 Machi 2025: Kuelekea wiki ya Wanawake Duniani, Vodacom Tanzania imewapa vyeti wasichana walioshiriki Program ya Code Like A Girl ambapo mabinti zaidi ya 3000 wamefanya program hiyo.
Akizungumza na Wanahabari wakati wa utoaji wa vyeti hivyo jana (Ijumaa) Meneja wa Mawasiliano na Matukio wa Vodacom Tanzania, Glory Mtui amesema kuwa wiki hii wamefikisha idadi ya zaidi ya mabinti 3000 ambao wamefanya program ya Code Like A Girl ambayo ni program waliyoifanya kwenye mikoa tofauti kama Mwanza, Arusha, Dar-es-Salaam, Mbeya na Dodoma. Aliendelea kusema;
“Ni program ambayo tumeifanya kwa kushirikiana na D Lab ambayo inaleta mabinti wenye umri wa miaka 14 mpaka 18, ambao wanakuja pamoja kwa ajili ya kujifunza masomo ya sayansi wanajifunza kutengeneza Website Cording na vitu vyote vinavyohusiana na STEM.
“Vilevile katika mafunzo haya wanapata nafasi ya kutoa mawazo yao, tofauti kwenye vile ambayo wanavitengeneza na kuonyesha kwa wenzao kwa ajili ya kupata maoni tofauti ili kujijenga zaidi.
“Katika mpango huu tumekuwa na mabinti na watu wenye  changamoto ya ulemavu wa kusikia na wengine hawana mikono ambao wanaandika kwenye kompyuta kwa kutumia miguu miguu yao, hivyo tumefurahi sana kwa kila mmoja wao kuja kufanya programu hii.” Alimaliza kusema Mtui.
Mkurugenzi wa Rasirimali Watu wa Vodacom, Vivienne Penessis akizungumza na mabinti hao waliohitimu aliwataja kujiamini kupitia ujuzi waliopata na wasiache kujiendeleza na kujiona kwakuwa wao ni wanawake hivyo hawana nafasi katika ushindani wa ajira. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN /GPL