The House of Favourite Newspapers

Mabondia wapima uzito, kupasuana kesho

0
Meneja wa Kamwamba, Craig Roussean (kushoto) akiwa na Rais wa TPBO, Abdallah Yassin ‘Ustadh’.

 

JUMLA ya mabondia sita  mapema leo wamepima uzito kwa ajili ya mapambano ya kimataifa ya ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati yatakayopigwa kesho  kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, Dar.

 

 

Mabondia hao ambao walikuwa wakitambiana kwa muda mrefu kabla ya kupima uzito kwa ajili ya mapambano hayo yatakayorushwa mubashara na Global TV Online kupitia website yake www.globaltvtz.com au www.youtube.com/user/uwazi1

 

Yohana Banda akipima uzito.

Katika tukio la kupima uzito ambapo alianza Mtanzania, Nasibu Ramadhani ‘Pacman’ aliyepata kilo 57, wakati mpinzani wake Yohane Banda kutoka Malawi akipata kilo 56. Wote wakiwa chini ya uzito waliosaini katika mikataba yao kitendo kilichoshangiliwa na mashabiki waliojitokeza kwenye zoezi hilo.

Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe akipima uzito.

Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ kwa upande wake alifanikiwa kupata kilo 60 sawa na mpinzani wake, Israel Kamwamba ambao  wakiwa nyuma kitendo ambacho kilipolekewa kwa shangwe kubwa kutoka kwa  wapambe wa kutoka kwa wapinzani wote.

Israel Kamwamba wa Malawi.

Furaha iliendelea kwa upande wa Mtanzania Idd Pialali ambaye alipata kilo 64  sawa na mpinzani wake kutoka DR Congo, Regin Championi ambapo muda mwingi alikuwa akitamba kumchinja mpinzani wake ndani ya raundi tatu.

Yohana akiendelea na vipimo.

 

Regin Champion.

 

Pialali akipima.

 

Regin Champion

 

Pialali akipima.

 

PICHA NA IBRAHIM MUSSA | GLOBAL TV

Leave A Reply