The House of Favourite Newspapers

Mabosi Simba kigugumizi usajili wa Mavugo

0

400554_386779341440791_392659364_nLaudit Mauvugo.

DIRISHA la usajili mdogo linatarajiwa kufunguliwa keshokutwa Jumapili lakini ndani ya Simba kuna sintofahamu juu ya nani hasa anatakiwa atoe kauli kuhusu mchezaji au wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa au kutemwa kikosini.

Ukweli huo unakuja kutokana na uongozi wa Simba kudai kuwa umemkabidhi kocha wao mkuu, Dylan Kerr, jukumu la usajili wa wachezaji wapya na wale atakaowatema, wakati huohuo Kerr naye anasema amekabidhi jukumu hilo kwa kamati ya usajili, hali ambayo inaonyesha kuna kurushiana mipira juu ya suala hilo.

Simba imekuwa ikitajwa kuwawania Paul Kiongera, Laudit Mauvugo na Kevin Ndayisenga huku ikidaiwa kuwa inaweza kuwatema Vicente Angban, Simon Sserunkuma, Pape N’daw na Emily Nimuboma ambao viwango vyao vimeonekana kuwa vya kawaida.

Rais wa Simba, Evans Aveva aliliambia gazeti hili kuwa wamepokea ripoti ya Kerr na wamepanga kuipitia kwa pamoja na Kamati ya Utendaji ya timu hiyo iliyopanga kukutana hivi karibuni.

Aveva amesisitiza kuwa hawataki kuingilia majukumu ya kocha katika suala hilo, ndiyo maana wamemuachia jukumu lote.

“Tumemuachia kocha kuamua wachezaji ambao hawahitajiki na wale tunaotakiwa kuwasajili,” alisema Aveva bila kufafanua juu ya kina nani watasajiliwa au kutemwa kikosini.

Akizungumzia suala la usajili, Kerr alisema jukumu hilo lipo katika Kamati ya Usajili inayoongozwa na Zakaria Hans Poppe.

“Nimeshaonyesha mahali penye makosa na panapostahili kufanyiwa marekebisho, sihusiki na suala lolote la usajili kwani tayari nimeshafanya kazi yangu na masuala hayo nimeyakabidhi kwa kamati ya usajili, kama kuna kitu waulizeni wao,” alisema Kerr.

Waandishi: Wilbert Molandi, Omary Mdose na Said Ally

Leave A Reply