Mabosi Simba Wawawahi Yanga Kigoma

SIMBA wamepanga kulipa kisasi, ni baada ya juzi Jumatatu baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo kuwasili mkoani Kigoma.

 

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

Katika kuelekea mchezo huo, Simba imepanga kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Mmoja wa mabosi wa Simba ameliambia, Championi Jumatano kuwa jumla ya wajumbe watano wa bodi hiyo, tayari wametua Kigoma kwa ajili ya kuandaa mazingira.

 

Bosi huyo alisema mabosi hao waliwasili na ndege mkoani hapo na moja kwa moja walielekea hotelini kabla ya kuanza kuweka mipango ya ushindi.

 

Aliwataja baadhi ya viongozi hao ni Mwina Kaduguda na Asha Baraka ambaye yeye ni mwenyeji wa mkoani huko.

 

“Simba wameonekana kuwa siriazi na mchezo wa FA, kikubwa wanataka kulipa kisasi baada ya kufungwa katika ligi.“Hivyo wamewawahi viongozi wa Yanga kwa kuwatanguliza viongozi wao mapema Kigoma kwa ajili kuandaa mipango ya ushindi ikiwemo kambi na uwanja wa kufanyia mazoezi,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Kaduguda kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Ni kweli tupo Kigoma, kama viongozi tumewahi kuandaa
kambi ya timu itakapofikia na
mambo mengine.”

STORI: WILBERT MOLANDI,Dar es Salaam


Toa comment