The House of Favourite Newspapers

Mabweni ya Wanafunzi Yatima Lateketea kwa Moto

0

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari African Muslim iliyopo Moshi Mjini Mkoani Kilimanjaro wamenusurika kifo baada ya kuzuka kwa moto na kuteketeza mabweni ya wanafunzi yatima wa shule hiyo.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inadaiwa kuwa moto huo ambao bado haujajulikana chanzo chake ulianza majira ya saa moja, ambapo wanafunzi wote walikua katika bwalo la chakula, hivyo moto haukuleta madhara kwa mwanafunzi yeyote lakini umeteketeza vifaa vyao vya masomo pamoja na nguo.

 

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaj Rajab Kundya ametoa pole kwa wanafunzi hao na kuwaahidi kuwa vyombo vya usalama vitafuatilia jambo hilo kwa umakini na kubaini chanzo cha moto huo na endapo itagundulika kuna yeyote aliyehusika na moto huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Kama tutabaini kunamtu aliyefanya hujuma ya kuchoma moto jela itamuhusu tu kwa namna yeyote, kama tutabaini ni uzembe tu, umetokea mahali basi yule mzembe atawajibika kwa uzembe wake,” DC Kundya.

Ikumbukwe kuwa, Septemba mwaka 2014, zaidi ya wanafunzi 96 wa Kidato cha nne katika Shule hiyo walinusurika kifo baada ya bweni lao, kuteketea kwa moto.

Leave A Reply