Madai ya Kupotezwa, Dimpoz Afunguka
Na BONIPHACE NGUMIJE| GAZETI LA IJUMAA|IJUMAA SHOW BIZ
MWANAMUZIKI Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ametoa povu kufuatia madai kuwa, hivi sasa kapotezwa na vijana wadogo wanaolazimisha ‘kuvaa viatu vyake’.
Akipiga stori na Showbiz, Dimpoz alisema hajapotea kwenye gemu kama mashabiki wanavyomchana mitandaoni na kwamba ukimya wake wa muda unatokana na yeye kujipanga katika kuandaa kazi mpya ili iweze kufanya vizuri atakapoiachia.
“Siyo kweli kuwa nimepotea, kwanza najiandaa kuachia kazi mpya ambayo ina ubora wa hali ya juu, wanaosema nimepotea wasubiri waone maajabu yangu,” alisema Dimpoz.