The House of Favourite Newspapers

MADAI YA KUTELEKEZA MTOTO, FAMILIA YA KIBA YATAKA DNA

 

DAR ES SALAAM: Wakati sakata la kudaiwa kutelekeza mtoto likishika kasi mitandaoni, familia ya mkali wa Bongo Fleva, Ali Salehe Kiba ‘Alikiba’ imepangua madai hayo na kumtaka mama wa mtoto huyo, ampime vinasaba (DNA) ili kubaini kama kweli ni damu yao.

 

Mapema wiki hii, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Hadija alitawala kwenye mitandao ya kijamii akishereheshwa na habari kuwa amempeleka Kiba Ustawi wa Jamii kwa kushindwa kumhudumia mtoto aliyezaa naye.

 

Awali, Risasi Jumamosi lilizungumza na rafi ki wa familia ya Kiba ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, akafunguka kwa kirefu kuhusu sakata hilo.

 

“Iko hivi, yule dada ni kweli alizaa na Kiba lakini si kwamba Kiba hataki kumtunza, la hasha! Kiba alikuwa akimhudumia tangu akiwa anaishi kwa mama yake.

 

“Hata hivyo, mtoto ana kama mwaka hivi alichukuliwa na akapelekwa kwa mama yake Kiba (bibi yake mtoto) akawa anahudumiwa kama watoto wengine,” alisema rafiki huyo.

 

Hata hivyo, rafi ki huyo aliweka bayana kuwa, Hadija ameibuka na suala la kumburuza msanii huyo ustawi kwa sasa baada ya kusikia anataka kufunga ndoa na mwanamke mwingine.

 

“Amesikia Kiba anataka kufunga ndoa na mwanamke mwingine, sasa eti anasema hataki mwanaye alelewe na mama wa kambo, kimsingi ni msumbufu tu,” alidai rafi ki huyo wa familia.

 

Risasi Jumamosi lilizungumza na dada wa msanii huyo, Zabibu Kiba ambaye alisema kwa sasa wameshaamua kumrudishia Hadija mwanaye na wanamtaka ampime DNA ili wajihakikishie kuwa ni damu yao.

 

“Sisi tumeshampa motto wake maana tulivyoona analeta hizi habari za sijui ustawi wakati mtoto anahudumiwa vizuri, tumeanza kupata mashaka hivyo lazima tujiridhishe kwanza,” alisema Zabibu.

 

Alipotafutwa na Risasi Jumamosi kuhusu suala hilo, Hadija alisema kwa sasa hawezi kuzungumza sana maana tayari suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria.

 

“Ni kweli hizo habari lakini kwa sasa siruhusiwi kuongea kwa kuwa suala hilo liko kwenye mikono ya sheria yaani liko ustawi wa jamii,” alisema Hadija. Alipotafutwa Kiba mwenyewe kuhusu suala hilo, simu yake iliita bila kupokelewa.

 

STORI: MWANDISHI WETU, RISASI

 

Sakata la Diamond Vs Basata, Baba Naye Afukua Makaburi!

Comments are closed.