Madai ya kuuza nyumba, mama Lulu awaka!

mamalulu

Mama mzazi wa staa grade one wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.

Imelda Mtema
Acheni hizo! Mama mzazi wa staa grade one wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, amewaka kufuatia madai ya kuuza nyumba ya aliyozawadia na mtoto wake huyo iliyopo Kimara- Saranga jijini Dar akisema kamwe hawezi kuiuza.

Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, mama Lulu alisema kuwa kuna madai mengi yamezuka kuhusiana na nyumba yake hiyo, jambo ambalo linamshangaza kwa sababu hana mpango wa kuiuza nyumba hiyo hadi anaingia kaburini.

IMG_0377 copy

….Akiwa na mwanaye.

Mama huyo aliongeza kwamba, alizawadiwa nyumba hiyo na mtoto wake, akiwa ameteseka kwa muda mrefu akiwa gerezani na alipotoka alimpa nyumba hiyo kama shukurani sasa iweje haiweke tena kwenye mikono ya madalali waiuze.

“Sina mpango wa kuuza nyumba yangu, naona watu wananitafuta sana, kwanza nitauzaje nyumba yangu ambayo nimezawadiwa na mtoto wangu ambaye amepitia kipindi kigumu sana? Nitakuwa wa ajabu sana kwa kweli,” aliwaka mama Lulu.

Mzazi huyo alisema kuwa kwa sasa anakwenda mara kwa mara kufanya usafi kwenye nyumba yake hiyo ili kuwafunga mdomo watu ambao wanaona kama ameitelekeza.

Loading...

Toa comment