The House of Favourite Newspapers

MADAI YA KUVUTA BANGI, KUONDOKA WCB…. HARMONIZE ABANWA!

Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’

DAR ES SALAAM: Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuagiza staa wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ kuchunguzwa na kukamatwa aendapo itathibitika ana­vuta bangi, mengi yameibuka.  

 

Mbali na hilo la bangi, pia kumeibuka tetesi nyingine mpya mitandaoni kuwa, jamaa huyo anataka kuondoka WCB iliyo chini ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa sababu kadha wa kadha hivyo Gazeti la Amani limembana ili kupata majibu kamili ya mambo hayo.

 

Kabla ya Harmonize kubanwa, kauli hiyo ya Makonda aliyoitoa wiki iliyopita al­ipokutana na wasanii wa kada mbalimbali kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, nayo ilichochea kuibuka kwa madai mengine mapya kuwa jamaa huyo anavuta sigara kupitiliza. “Ukitaka kuamini tembelea hata ukurasa wake wa Instagram, utakutana na picha kibao akipuliza fegi au ameshikilia vipisi vya fegi na kutoa moshi kama treni ya mizigo.

 

“Kuna siku hata yeye mwenyewe aliposti picha akivuta sigara na kuandika kuwa ameathirika na sigara,” alisema mmoja na watu wa karibu wa Harmonize mitandaoni na kuongeza: “Kuhusu bangi, sina uhakika, lakini kwa sigara, jamaa ni noma. Anaweza hata akawa anamaliza pakti mbili kwa siku. Wenyewe wanamwita ‘chain smoker’.”

 

Kwa mujibu wa vyanzo vya mitandaoni, Harmonize yupo mbioni kuondoka Wasafi kwenda kujenga himaya yake baada ya ku­jiona amekuwa mkubwa na sasa anaweza kujitegemea. “Harmonize sasa amekua kiuchumi, amemkaribia bosi wake, Diamond, kuon­doka ni suala la muda tu kwani suala lake ni nyeti sana pale WCB,” kilisema chanzo kingine na kuongeza:

 

“Mwaka jana (2018) Harmonize alifanya vizuri mno, inawezekana hata zaidi ya Dia­mond. Kuna tetesi naye anataka kujitanua kwa kuanzisha lebo yake na kusajili wasa­nii wake kama Diamond.”Kufuatia unyeti wa madai hayo, Amani lilimtafuta Harmonize na kumbana ambapo mbali na kukanusha kuvuta bangi pia alitia ngumu kufungukia ishu ya kuondoka WCB.

“Sivuti bangi, lakini sitaki kuzungumzia mambo hayo,” alisema Harmonize kisha akakata simu. Alipotafutwa mmoja wa mameneja wa WCB, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ aliomba ampigie simu mwandishi wetu baadaye, lakini hakufanya hivyo na hata alipotafut­wa tena na tena, simu yake iliita bila kupokelewa.

 

Si mara ya kwanza kwa Harmonize kudaiwa kutaka kuondoka WCB. Mwaka 2017, staa huyo alilazimika kukanusha taar­ifa zilizokuwa zimesambaa zikimhusisha yeye kuondoka kwenye lebo hiyo inayosi­mamiwa mastaa wengine kama Rayvanny, Lavalava, Mbosso na Queen Darleen. Harmonize anadaiwa kutaka kusepa ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipoondoka Rich Mavoko na kwenda kujitegemea

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.