The House of Favourite Newspapers

Madaktari 500 wa Tanzania Wakataliwa Kenya

Katibu Mkuu wa KMPDU, Ouma Oluga.

UMOJA wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umepinga vikali hatua ya Serikali ya Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya ina madaktari wengi ambao hawaajiriwa.

Katibu Mkuu wa KMPDU, Ouma Oluga umepinga hatua hiyo na kudai kuwa Serikali ya Kenya haijawa makini katika kushughulika na tatizo la upungufu wa madaktari nchini humo

Akizungumza na mtandao wa The Star wa nchini Kenya siku ya Jumamosi, Oluga alisema

“Kenya ina zaidi ya madaktari 1,400 ambao wanasubiria ajira. Itakuwa gharama kubwa na dalili ya kushindwa kutumia fedha za umma vizuri kwa kuwa na madaktari 500 wa kitanzania kwa gharama ya Shilingi 20,000 kwa siku,” amesema.

Oluga amesema kuwa Kenya inapaswa kupitia upya utaratibu wake wa Rasilimali Watu kwa mujibu wa miongozo ya Afya kama ambavyo KMPDU imekuwa ikihitaji hapo kabla.

Comments are closed.