The House of Favourite Newspapers

MADAM RITA AMLILIA CASSIAN

Rita Paulsen ‘Madam ‘Rita’

JAJI Mkuu wa Shindano la Bongo Star Search, Rita Paulsen ‘Madam ‘Rita’ amesema kuwa amesikitishwa na ugonjwa wa aliyekuwa Mshindi wa BSS 2009, Pascal Cassian na kuahidi kumsaidia.  

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Madam Rita alisema kuwa ana muda mrefu hajaonana na msanii huyo anayeimba injili kwa sasa hivyo alivyopewa taarifa ya kupata ajali alishtuka na kusema atafuatilia ili aone namna ya kumsaidia.

“Niliambiwa na mfanyakazi wangu mmoja baada ya kuona kwenye gazeti, kwa kweli niliumia sana, nitaenda kumuona na kumsaidia chochote, naamini atapata matibabu mazuri na atapona,” alisema Madam Rita. Hivi karibuni Cassian aliripotiwa na Gazeti la Uwazi kuwa ni mgonjwa akisumbuliwa na kibofu baada ya kupata ajali mbaya

STORI: Imelda Mtema, Dar

Part 2: MSHINDI BSS – “Madam Ritta Nakufa mimi nisaidie”

Comments are closed.