The House of Favourite Newspapers

Madam Sophey Charity Movement yatoa msaada Shule ya Jangwani

0

1Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisiya Madam Sophey Charity Movement, Sophia Mbeyela (kulia )akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani ambaye ni mlemavu wa viungo.Anayeshuhudia ni mwalimu wa shule hiyo,Rabia Kimaro.

2Sophia Mbeyela (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi aliokuwa ameambatana nao shuleni hapo.

3Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani.

4Wanafunzi wa kimsikiliza Mbeyela (hayupopichani).

5Walioko mbele kutoka kushoto ni Mratibu wa Maktaba ya Taifa,Mwalughelo Lusekelo, Sophia Mbeyela na Mwanzilishi wa Wives Cooking Club, Miliam Lukindo.

6Mbeyela akizungumza jambo mbele ya wanafunzi hao.

7Mhazini wa Tanzania Action For Disabled Uk, Flora Mwakasege.

8Sophia Mbeyela (mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau aliokuwa ameambatana nao sambamba na wanafunzi wa Shule ya Jangwani.

9

Wanafunzi wa shule hiyo‘wakijiselfisha’na mmoja wa watu walioambatana na Sophia.

MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Madam Sophey Charity Movement ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho ya jijini Dar, Sophia Mbeyala, leo Ijumaa ametoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali katika Shule ya Sekondari Jangwani, Dar.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mbeyela amesema kuwa taasisi yake hiyo siyo ya kiserikali, lakini inajihusisha na uhamasishaji kwa watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu katika kufanya maendeleo kwenye jamii.

Akiwa shuleni hapo, Mbeyela amesema kuwa lengo kubwa la kutoa msaada huo ni kuwatia moyo wanafunzi wenye ulemavu na hata wasiokuwa na ulemavu waweze kujiona wako sawa kama watu wengine na kuwahimiza kusoma vitabu ili hapo baadaye waweze kuwa mabalozi wazuri.

“Mnaweza kujifunza kupitia mimi, sikuweza kukata tamaa wala kukatishwa na mtu yeyote, nilihakikisha ninasoma kwa bidii na hadi nikaja kuwa mwalimu, hivyo niwaombeni wanafunzi mlio na ulemavu wa viungo msikate tamaa kwa kujiona hamuwezi, someni kwa bidii na mtaweza kufanikiwa kama mimi au zaidi,” alisema Mbeyela.

Mbeyela aliongeza kuwa msaada huo alioutoa umetokana na juhudi zake binafsi huku akiongeza kuwa na yeye pia alipewa kama msaada kutoka katika udhamini wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Tanzania Action For Disabled UK, huku akisema kuwa zoezi hilo ni mwendelezo wake ulioanza wiki iliyopita ambapo aligawa vitabu katika shule mbalimbali za jijini Dar.

Miongoni mwa shule hizo ni Makumbusho na Turiani ambazo zote ni za sekondari.

Leave A Reply