The House of Favourite Newspapers

Madee Ampa Neno Kali Mchumba Mpya wa Dogo Janja

0

RAPA maarufu nchini, Hamad Ally ‘Madee’ amemweleza mpenzi mpya wa kijana wake, Dogo Janja aitwaye Quenlinnah kwa kumwambia ategemee mengi kwa sababu yupo kwenye mahusiano na mtu maarufu.

 

Madee amesema hayo baada ya Dogo Janja kumvalisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo siku ya juzi Februari 10, 2020, kwenye boti wakati wakirejea jijini Dar es Salaam wakitokea Visiwani Zanzibar.

 

“Mpenzi wa Dogo Janja ajue kabisa yupo kwenye mahusiano na mtu maarufu na yeye anaelekea kuwa maarufu muda sio mrefu, kwahiyo asisikilize maneno ya watu na ategemee mengi ambayo yatatikisa mahusiano yao ambayo ni mapya,” amesema Madee.

 

Aidha, katika msimu huu wa wapendanao Dogo Janja mwenyewe amesema; “Msimu wa mapenzi umekuwa mzuri kwetu kwani nimeufurahia sana mimi na mpenzi wangu kule visiwani Zanzibar, nikiwa na familia yangu kama Linah, Recho na Madee”.

Leave A Reply