MADEE: RAHA ILIYOJE KULEA MTOTO
WAKATI wanaume wengi wakisifika kwa kukwepa kulea watoto wao, kwa mwanamuziki wa kitambo kwenye gemu ya Bongo Fleva, Hamady Ally, ‘Madee’ kwake hiyo wala si ishu, anapenda kinoma ulezi.
Usije ukashangaa siku ukimuona akiwa kitaa na wanaye mdogo aitwaye Chonge, ukadhani kasusiwa na mama mtoto, wala! Kaamua mwenyewe kuwa karibu na mwanaye huyo ili amzoee.

Madee aliliambia Risasi Mchanganyiko hivi karibuni kuwa: “ Hakuna kitu kinanipa raha kama ninavyomlea mtoto wangu, yaani nikimuona ananipa nguvu nyingi ya kutafuta pesa ili aweze kukua katika maisha bora yeye na dada yake.”
IMELDA MTEMA


Comments are closed.