The House of Favourite Newspapers

Madee: Sijaishiwa Ubunifu

Hamadi Ally ‘Madee’

Na ALLY KATALAMBULA| GAZETI LA AMANI| SHOW BIZ XTRA
Rapa
asiyechuja kwenye sayari ya muziki wa Bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ya ‘Helaa’ Hamadi Ally ‘Madee’ amesema kitendo cha kutoa wimbo wenye maudhui yanayo izungumzia pesa hajaishiwa ubunifu.

Akichonga na Amani Madee alisema kuwa ni upeo mdogo wa kuelewa mambo kutoka kwa baadhi ya wadau wa muziki wa Bongo fleva kumzodoa kuwa wimbo huo hauna jipya kwakuwa tu maudhui yake yanafanana na ngoma iitwayo ‘Pesa’ aliyowahi kuimba na Tunda mani.

Hamadi Ally ‘Madee’

“Sijaishiwa ubunifu, pesa inauwanja mkubwa wa kuzungumziwa,naweza nikaeleza na kueleza na nisifike tamati, kwani nyimbo za mapenzi Duniani zipo ngapi tangu zianze kuimbwa? mbona hakuna aliyerudia mashairi yakafanana. Pesa nimeleza ilivyo ngumu kuipata, utakavyoipata na matumizi yake” Alisema Madee

Comments are closed.