The House of Favourite Newspapers

MADEREVA WAANZA KUTENGENEZA VYETI FEKI, POLISI WAWASHTUKIA

Jeshi la Polisi Nchini limesema limepata taarifa za uwepo wa madereva wa magari ya abiria ambao wameanza kutengeneza vyeti bandia vinavyowatambulisha kupitia mafunzo ya udereva wakiwa na lengo la kukwepa zoezi la kurejea darasani na kupata mafunzo kwa mujibu wa sheria.

 

Taarifa hii inakuja wakati madereva wanaofikia 350 Mkoani Arusha waliojisalimisha Polisi kwa kosa la kujipatia leseni pasipo kufuata taratibu sahihi za mafunzo ya udereva wakiwa wamepatiwa kozi maalumu ya majuma mawili iliyoendeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi VETA.

 

Jeshi la polisi limesema kumezidi kujitokeza idadi kubwa ya madereva waliopata leseni kwa njia za mkato wakimiminika kwenye ofisi za jeshi hilo kujiandikisha kwa ajili ya mafunzo ya udereva na kwamba jambo hilo linatoa matumaini ya kupungua kwa athari zinazosababishwa na madereva wasio na taaluma kamili.

Comments are closed.