The House of Favourite Newspapers

Madereva Walevi Kupimwa Kilevi Kwa Mashine Pwani

0
ajali za magari
Ofisa wa usalama barabarani, Peter Buyi ‘Wakwetu’ akimpima kilevi dereva wa lori la mchanga eneo la Kibaha Pwani
Mratibu Msaidizi wa Polisi (RTO) Mkoa wa Pwani, Salum Morimori, akiongea na waandishi wetu (hawapo pichani) eneo la oparesheni waliyoianzisha ya kupima kilevi madereva.
Ofisa usalama barabarani akimpongeza dereva wa daladala baada ya kumpima na kumkuta hana kilevi.
… akisimamisha gari kwa ajili ya ukaguzi
Ofisa wa usalama barabarani akiwa akimpeleka dereva sehemu ya kulipia faini baada ya kukutwa na makosa.

KATIKA hatua ya kukomesha ajali za magari mkoani Pwani imeamua kuwapima kilevi madereva wote wanaopita mkoa huo.
Zoezi la kuwapima madereva hao limefanyika tangu jana asubuhi maeneo ya Mizani Kibaha- Maili Moja likiongozwa na Mratibu Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Pwani (RTO) Salum Morimori.

Lengo la kuwapima madereva hao ulevi ni kukomesha au kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikisababishwa na madereva hao kizembe.
“Unajua ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa kizembe na baadhi ya madereva kwa kunywa pombe na baadhi yao kuvuta bangi kwa madai kuwa wanapata (starter) ‘mori’. Sasa nasema ole wao, ”alisema kamanda huyo.

Akiongea na waandishi, Morimori alisema zoezi la kuwapima madereva walevi litakuwa endelevu katika mkoa huo na hatawafumbia macho madereva wazembe, walevi na wanaoendesha magari kwa mwendo kasi.

Aidha aliwataka madereva wote wa magari madogo, malori, daladala, na mabasi yanayoenda mikoani na nje ya nchi kutokupita katika mkoa huo wakiwa wamelewa.

“Dereva yeyote yule akijiona amekunywa pombe au amevuta bangi namuomba sana kama anataka kusafiri kwa amani basi aahirishe safari yake na asikanyage katika mkoa wangu wa Pwani, “ alisisitiza kamanda huyo.

NA ISSA MNALLY/RICHARD BUKOS/GPL

SHUHUDIA MADEREVA WAKIPIMWA KILEVI

Chadema: Lissu Amevunjwa Mguu na Nyonga Lakini Jasiri, Tumuobee!

 

Leave A Reply