The House of Favourite Newspapers

Madhara sita ya kutoa mimba

0

01Leo tuzungumzie madhara sita ya kutoa mimba na madhara yake kama tutakavyoona hapa leo.

UNAWEZA KUPOTEZA UHAI
Ukitoa mimba unaweza kupoteza maisha kutokana na ukweli kwamba mara nyingi ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba mwanamke anaweza kuvuja damu sana, au kupata madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi.

WATOTO KULEMAA UBONGO
Utoaji wa mimba huaribu mlango wa mfuko wa uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya muda (njiti). Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kujikuta wakipata ulemavu wa ubongo maisha yao yote.

MIMBA NJE YA KIZAZI
Mfuko wa uzazi una utando maalumu ambao hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo Fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mfuko wa uzazi. Lakini utoaji wa mimba huathiri mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi.

KANSA YA KIZAZI
Wanawake wengi waliowahi kutoa mimba wanapoteza uwezo wa kuzaa, hivyo kuwa wagumba. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka kwani mfuko huwa na kovu.

KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA
Baadhi ya wanawake waliowahi kutoa mimba, hujutia kitendo hicho, hivyo kuathirika kisaikolojia. Wengine huweza kusikia sauti ya mtoto akilia wakati hakuna mtoto huyo jambo linalowaweka katika mazingira magumu.

Kufautia hali hiyo, hujikuta wakishindwa kuwa na ufanisi mzuri wa kazi na masuala mengine ya kijamii.

Leave A Reply