The House of Favourite Newspapers

Madhara ya pombe kwenye ubongo

KUPOTEZA fahamu kutokana na unywaji wa pombe kupita kiasi ni hali ambayo watu wengi wameshawahi kuishuhudia japo mara moja maishani.

Kupoteza fahamu kutokana na unywaji wa pombe ni nini?

Hii ni hali ya ubongo kushindwa kunakili kumbukumbu ya mambo yanayofanyika katika mazingira ya mtu anapokuwa mlevi.

 

Kwa mujibu wa taasisi ya kitaifa ya kukabiliana na matumizi mabaya ya vileo, hali hiyo hutokea kwa sababu mzunguko katika eneo la ubongo uliyo na jukumu muhimu la kuimarisha kumbukumbu za maisha yetu ya kila siku, imefungwa na pombe.

 

Dk Kate Carey, Profesa wa Sayansi ya Tabia za Watu katika jamii kutoka Chuo Kikuu cha Brown huko Providence, Rhode Island anasema: “Kati ya asilimia 30 hadi 50 ya vijana ambao wanakunywa pombe wameripotiwa kuwa na hali ya kupoteza fahamu kutokana na ulevi.”

 

Ni watu gani wako katika hatari ya kupoteza fahamu kutokana na unywaji wa pombe? Utafiti umebaini kuwa watu walio na miili midogo hukabiliwa na hali ya kupoteza fahamu hasa wanapokunywa pombe kupindukia.

Wanawake pia hukabiliwa na hali hiyo kwa sababu viwango vya pombe hupanda haraka kwa wanawake kadiri wanavyokunywa pombe bila kunywa maji.

Hali ya mtu pia inaelezea ni kwa nini watu wengine hupoteza fahamu wanapokunywa pombe kupindukia na wengine kutoelewa walichokifanya baada ya kulewa.

Baadhi ya wataalam pia wanasema wale watu wanaovuta sigara huku wakinywa pombe wako katika hatari ya kupoteza fahamu kutokana na ulevi.

 

Je, kuna dalili zozote hujitokeza?

Mtu anaweza kujieleza vizuri akiwa mlevi na hata kujua njia ya kwenda nyumbani akiwa mlevi, lakini baadaye akasahau alichokifanya.

Dk Carey anasema: “Ukimuuliza mtu aliyekuwa mlevi jinsi alivyofika nyumbani hakumbuki nini kilichofanyika alipokuwa mlevi.”

Mlevi wakati mwingine huchanganyikiwa kadiri kiwango cha kileo kinavyoongezeka mwilini mwake. Kwa mfano hawezi kuendelea na mazungumzo.

 

MADHARA YA UNYWAJI POMBE NI YAPI?

Kwa mujibu wa Kituo cha Marekani cha masuala ya ulevi na madhara yake, watu wanaweza kujiingiza katika tabia ambazo hawana wakiwa katika hali za kawaida.

Ukiwa mlevi, inakuwa rahisi kwako kudhulumiwa kwa njia mbalimbali. Wakati huohuo, unaweza kuhatarisha maisha ya wengine. Kwa kufanya mambo ambayo hungefikiria kufanya ukiwa na akili timamu.

Mara nyingi mlevi huwa hakumbuki yale yaliyojiri siku iliyotangulia alipokuwa amelewa chakari. Hii inatokana na hali ya yeye kupoteza fahamu.

 

USHAURI

Hata hivyo, hali ya kupoteza fahamu mara kwa mara mtu akinywa pombe huenda ni ishara ya tatizo la kiafya ambalo huenda likasababisha maradhi ya ini.

Hivyo ukipoteza fahamu na hunywi pombe, haraka sana nenda ukamuone daktari akupime na akigundua tatizo atakupa dawa stahiki.

Na Mtaalam Wetu, A.Mandai

SIMU: 0716 300 200

TID: “Wasafi Festival Inahitaji Mnyama kama Mimi”

Comments are closed.