Madiwani wa Buchosa Watembelea Bungeni, Shigongo Awapokea

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na madiwani mbalimbali wa kata zilizopo Jimbo la Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza na Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (katikati nyuma ya Naibu spika mwenye tai nyekundu).

Madiwani mbalimbali wa kata zilizopo Jimbo la Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza, leo Alhamisi Juni 10, 2021 wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma na kupokelewa na mbunge wao, Eric Shigongo.

 

Wakiwa bungeni, madiwani hao wametambulishwa na Naibu Spika, Dkt. Tulia Akson kisha baadaye, wakiwa nje ya ukumbi wa bunge wakapata fursa ya kuzungumza na Shigongo, wabunge wengine, mawaziri na manaibu waziri pamoja na naibu spika kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika kata zote za Jimbo la Buchosa.

Madiwani mbalimbali wa kata zilizopo Jimbo la Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza wakisalimia bungeni.

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (kulia mwenye kibegi) akiongea na wageni wake bungeni.

 Tecno


Toa comment