Madiwani Waomba Ujenzi wa Barabara Zisizopitika Zifanyiwe Ukarabati Mtama
Madiwani waomba ujenzi wa barabara zisizo pitika zifanyiwe ukarabati ili ziweze kupitika kwa urahisi na wakulima waweze kusafirisha mazao yao bila shida.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama Abdalla Tipu amewaomba madiwani wanaporudi kwenye kata zao waende wakafanye mikutano na kusimamia maendeleao.
Tipu ameyasema hayo katika kikao cha Madiwani cha robo ya kwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ya Mtama pia tarifa za kato zote 20 za halmashauri hiyo ziliwasilishwa.
“Madiwani tuendelee kufanya vikao kwenye kata zetu twendeni tukafanye kazi.Wakuu wa idara tunapoona miradi haikamiliki sisi kwetu ndiyo fimbo ya wananchi kutupigia kwahiyo tunaomba mambo yaende kama miradi ya maji basi itekelezwe kwa wakati”.amesema Tipu.
Baadhi ya madiwani walielezea changamoto zinazo wasumbua katika maeneo yako hasa kilio chao kikielekea kwenye uchakavu wa miundo mbinu ya barabara na kuiyomba mamlaka husika kutatua kilio hicho.
Diwani Kata ya Mnolela Omary Liveta amesema Halmashauri hiyo ina changamoto sana katika miundo mbinu ya barabara kila siku wanapewa taarifa ya kuanza miradi lakini haitekelezeki.
“Changamoto ya barabara kwenye Halmashauri yetu tunapewa matangazo lakini hatujui ni lini utaanza tunawaita wananchi tunawapa taarifa lakini hatujui ni lini utaanza wananchi wanatuona sio wa kweli. amesema Liveta.
Kwaupande wake diwani wa Nyangao Mohammed Babu ameomba kujengwa kwa barabara ya Nyangao kwenda Namupa kwasababu haipitiki hata namna ya kutoa korosho kupeleka ghalani ni changamoto.
“Barabara ya Nyangao kwenda Namupa haipitiki hata kwa Trekta na kule kuna upimaji wa korosho hatu jui hata zitatokaje huko ziliko”alisema Babu.
Kaimu meneja Wakala wa baraara za mijini na vijijini(Tarura)Baraka Ojisa alisema baadhi ya barabara alishaoneshwa mkandarasi na wakati wowote kazi itaanza.
“Barabara Mnolela hadi Simana nikweli tulimuonesha makandarasi eneo la kazi utaratibu kuna siku 14 zakujiandaa baada ya kukabidhiwa kazi wiki hii ni ya pili wiki ijayo tunaamini kazi itaanza”amesema Baraka
Baraka liongeza kwakusema barabara ya Namupa hadi Mihima mradi huu umebakia kutanganzwa ila wiki ijayo tutaangalia nana gani tunaweza kufanya ili barabara iyanze kupitika.