Madrid, Barcelona Hatihati Kucheza UEFA

IMERIPOTIWA kuwa kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) lipo mbioni kutoa adhabu kwa Real Madrid, Barcelona na Juventus baada ya kushindwa kujitoa kwenye Super League.

Real Madrid, Barcelona na Juventus zilisalia kwenye mchakato huo huku timu kama Arsenal, Liverpool, Inter Milan, Tottenham, Chelsea, AC Milan, Man United na City wao walijitoa na kuomba radhi.

 

UEFA wiki hii ilithibitisha kuwa klabu tatu zitachukuliwa hatua za kinadhamu kutokana na kuendelea kuwa kwenye mchakato.

Taarifa ya UEFA ilisema: “Uchunguzi umefanyika na kitengo cha maadili na nidhamu cha UEFA kuwa uchunguzi umefanyika kuhusu Super League kwamba hatua za kinidhamu kwa Madrid, Barcelona na Juventus.

 

Na taarifa za hatua zitakazochukuliwa zitawekwa wazi.” Hata hivyo adhabu hizo zitatolewa kwa Madrid, Barcelona na Juventus ambao huenda wasishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu mmoja au miwili na kupigwa faini.

 

Kwa maana hiyo huenda msimu ujao Real Sociedad na Real Betis zikachukua nafasi ya Madrid na Barcelona UEFA.


Toa comment