The House of Favourite Newspapers

Madrid Kumuuza Varane Manchester United

0

KLABU ya Real Madrid, imesema haitamuongezea mkataba beki wake, Raphael Varane, huku ikiwa na mpango wa kumuuza nyota huyo kwa pauni 43m.

 

Varane kwa sasa anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na Klabu ya Manchester United, huku kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer akionekana kukomalia dili hilo, kama akishindwa basi watageukia kwa Pau Torres wa Villarreal.

 

Man United kwa sasa inasaka beki ambaye atakuwa msaada kwenye safu yao ya ulinzi akisaidiana na Harry Maguire, hiyo ni baada ya Victor Lindelof kuonekana hajawafiti.

 

Kuondoka kwa Varane ndani ya Madrid, litakuwa pigo lingine kwao ikiwa ni baada ya Sergio Ramos kumaliza mkataba wake na kuagwa.

Leave A Reply