The House of Favourite Newspapers
gunners X

Madrid Yaichapa Girona 6-3, Ronaldo Yupo On-Fire, Atupia Nne

 

KLABU ya Real Madrid wakiwa nyumbani wameinyuka timu ya Girona kwa mabao 6-3 katika mechi ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga Santanda’ jana Jumapili, Machi 18, 2018 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

 

Katika mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake Ronaldo aliandika rekodi nyingine baada ya kugonga ‘hat trick’ ya 50 katika maisha yake ya soka kwa kutupia mabao 4 kambani.

 

Ronaldo aliweka wavuni mabao yake kunako dakika ya 11, 47, 64 na ya 90+1, huku Lucas Vazquez akiifungia Madrid bao la 5 dakika ya 59 na Bale dakika ya 86.

Kwa upande wa Girona mabao yao yalifungwa na Stuani dakika ya 29 na 67 na Juanpe dakika ya 88 mchezo huo.

Kwa ushindi huo, Ronaldo amefikisha mabao 22 ya Laliga mbele ya Suarez mwenye mabao 21 huku Messi akiongoza kwa kuwa na mabao 25.

Madrid wanabaki nafasi ya tatu katika ligi hiyo wakiwa na pointi 60 nyuma ya Atletico Madrid wenye pointi 64 na vinara Barcelona wakiongoza kwa pointi 75.

 

 

Real Madrid (4-4-2): Navas; Carvajal, Varane, Nacho, Marcelo; Lucas Vazquez, Kovacic (Modric 70), Kroos, Asensio (Bale 70); Benzema (Isco 83), Ronaldo

Unused subs: Casilla, Theo H., Vallejo, Casemiro

Goals: Ronaldo 11, 47, 64, 90+1, Lucas Vazquez 59, Bale 86

Bookings: Carvajal 52, Granell 90+3

Girona (3-4-2-1): Bono; Ramalho, Bernardo, Juanpe; Maffeo (Aday 83), Pere Pons, Granell, Mojica; Portu, Borja Garcia (Lozano 69), Stuani (Olunga 87)

Unused subs: Iraizoz, Muniesa, Copovi, Aleix Garcia

Goals: Stuani 29, 67, Juanpe 88

Booking: Mojica 30.

BANDA: Wachezaji wa Tanzania Hawana Wivu wa Kimaendeleo

Comments are closed.