The House of Favourite Newspapers

Video: Maelfu ya raia nchini Iran Wauaga Mwili wa Aliyekuwa Rais wa nchi Hiyo

0


Maelfu ya raia nchini Iran wamelizunguka Jeneza lililokuwa limeubeba mwili wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi aliyefariki Dunia kwa ajali ya helikopita wiki iliyopita.

Gari iliyokuwa imeibeba miili ya Ebrahim na viongozi wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo ilipita katika mji wa Tabriz Kusini Magharibi mwa Iran kwa ajili ya kutoa heshima ya mwisho.

Kiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei,amemteua Makamu wa Rais kuwa Rais wa muda ukisubiriwa uchaguzi ambao utafanyika mwei Juni mwaka huu.

Hadi kufikia sasa Serikali ya Iran haijataja chanzo cha ajali ya helikopia iliyoanguka katika Milima mirefu yenye ukungu mwingi lakini uchunguzi ukiwa unaendelea kufanyika.

Leave A Reply