Maelfu ya Wasauzi Wamshangilia JPM Akiwasili Uwanjani – Video

Shangwe na nderemo zikirindima wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa leo Jumamosi, Mei 25, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt Jakaya Kikwete, leo Mei 25, wameungana na wananchi zaidi ya 30,000 wa Afrika Kusini na marais 22 wa mataifa mbalimbali duniani kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa katika Uwanja wa Loftus Versfeld, Pretoria.

Magufuli na Kikwete waliondoka jana nchini pamoja na Naibu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) – Bara, Phillip Mangula kushuhudia uapisho huo wa Maphosa mabye leo amekuwa Rais wa tano wa Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alivyowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa leo Jumamosi, Mei 25, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alivyowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

TAZAMA TUKIO ZIMA LA KUAPISHWA KWA RAMAPHOSA


Loading...

Toa comment