The House of Favourite Newspapers

Mafuriko Dar: UDART Wasitisha Usafiri wa Mwendokasi

 

Taarifa kwa Umma

Kufuatia kujaa maji juu ya daraja la Mto Msimbazi kwenye Barabara ya Morogoro na kusababishwa kufungwa kwa muda kwa barabara hiyo, Kamapuni inayotoa huduma katika mradi wa Mabasi yaendayo haraka jijini Dra es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART) inauarifu umma kuwa huduma za mabasi hayo zimesitishwa kwa muda kuanzia saa 3:00 asubuhi ya Januari 08, 2018.

 

Mara baada ya hali kutengemaa na mamlaka husika kuruhusu barabara hiyo kuendelea kutumika, huduma zitarejea mara moja. Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Deus Bugaywa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART.

Comments are closed.