The House of Favourite Newspapers

Mafuriko Yasababisha Vifo vya Watu Zaidi ya 600 Nchini Nigeria

0
Mafuriko yalivyoathiri maeneo mbalimbali nchini Nigeria

NCHI ya Nigeria imekumbwa na mafuriko ambayo yamevunja historia kwa nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 10 ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 600.

 

Zaidi ya watu milioni 1.3 wamehama makazi yao na wengine zaidi ya laki mbili makazi yao yameharibiwa na madhara yaliyosababishwa na mafuriko hayo.

 

Aidha mafuriko hayo yanasadikika kuendelea hadi mwisho wa mwezi Novemba.

Miundombinu mingi imeharibika vibaya kutokana na madhara yaliyosababishwa na mafuriko nchini Nigeria

Nchi ya Nigeria imekuwa ikikumbwa na mafuriko ya kila msimu lakini mwaka huu mafuriko hayo yamekuwa ya kiwango kikubwa kuliko miaka yote.

 

Kutokana na madhara yaliyosababishwa na mafuriko hayo kumekuwa na hofu kubwa juu ya upatikanaji wa huduma za kijamii kama chakula na usambazwaji wa nishati ya mafuta.

Leave A Reply