The House of Favourite Newspapers

Mafuriko yaua 13 Ufaransa

0

 

2

Baadhi ya maeneo nchini Ufaransa yaliyokumbwa na mafuriko.

1

Mechi kati ya Nice na Nantes ililazimika kuvunjika kutokana na mvua kubwa zilizopelekea mafuriko.

3

Stesheni ya treni ikiwa imejaa maji na kuharibu miundombinu.

4

Madhara ya mafuriko hayo katika mitaa ya Nice, Ufaransa.

5 6

Baadhi ya magari yaliyosombwa na mafuriko.

Takriban watu 13 wapoteza maisha huko kusini mwa Ufaransa baada ya mvua iliyoandamana na upepo mkali kusababisha mafuriko eneo hilo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu sita hawajulikani walipo mpaka sasa.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kuwa zaidi ya mililita 175 za mvua zilinyesha ndani ya saa mbili jana usiku.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amevishukuru vikosi vya uokoaji na kuwaomba Wafaransa kuwa na mshikamano wa kitaifa katika kipindi hiki na anatarajia kwenda kutembelea maeneo yote yaliyokumbwa na mafuriko akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Bernard Cazeneuve.

 

Leave A Reply