The House of Favourite Newspapers

Wizi Ofisi ya Kamishna Mkuu TRA… Magari 2 Yakamatwa

0

Sirro

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Simon Sirro.

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari mawili yakihusishwa na wizi katika ofisi ya kamshina mkuu wa TRA huku yakiwa na vifaa vilivyoibiwa katika ofisi hiyo vikiwa ni pamoja na komputa, na TV.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda Simon Sirro amesema kutokana na oparasheni kali iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi ilifanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa wanne wakiwa na vifaa vilivyoibiwa.

Aidha kamanda huyo wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema katika oparesheni hiyo pia jeshi la polisi lilifanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 150 mali ya Bw Ahmed Huwel mkazi wa Msasani.

Katika hatua nyingine Kamanda Sirro ametangaza kusitishwa kwa muda kwa shughuli za ulinzi shirikishi katika vituo vya polisi kutokana na vikundi hivyo kualamikiwa na wananchi kwa kutokuwa na tija katika jamii.

Source: ITV

Leave A Reply