The House of Favourite Newspapers

Magari yaliyoibiwa London yakamatwa Uganda

0

magari (2)

Njia ambayo magari hayo ya wizi yalisafirishwa toka London, Uingereza hadi Kampala, Uganda.
magari (1)Gari aina ya Audi TT iliyosajiriwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).magari (5)Lexus lilokuwa limeibiwa Londoni na kupelekwa Kampala, Uganda.
magari (4)

Polisi wa Uganda wakikagua magari hayo.

Kampala, Uganda

Wapelelezi wa Kimataifa wamekamata gari aina ya Lexus liliyoibiwa London, Uingereza na kusafirishwa hadi Kampala, Uganda. Gari hilo lilikutwa likiwa limefichwa pamoja na magari mengine hutengenezwa nchini Uingereza yenye thamani  ya Euro 1,000,000 sawa na shilingi 2,440,000,000.

Shirika la Kudhibiti Uhalifu nchini Uingereza (National Crime Agency) waliweza kutumia programu maalum ya simu ya mkononi (smartphone app) na kufuatilia njia ambazo gari hilo RX450h lilisafirishwa hadi kufika Uganda umbali wa maili 6,000.

Baada ya kufika eneo ambalo gari hilo lilikuwa limefichwa, maofisa wa National Crime Agency walikuta magari mengine 28 ya lexus yaliyoibiwa siku za nyuma na wauza magari ya magendo na kuyasafirisha hadi Mji Mkuu wa Uganda, Kampala.

Programu hiyo inaonesha kuwa, gari hilo baada ya kuibiwa Uingereza lilipita Le Havre, Ufaransa, Oman, baadaye Mombasa Kenya kabla ya kushushwa Kampala, Uganga likiwa kwenye kontena maalum la chuma.

Programu hiyo imeweza kuonesha pia namna ambavyo maofisa wa polisi nchini Kenya na Uganda walivyoruhusu magari hayo kuvuka mipaka na kuingia nchini mwao.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ni zaidi ya magari 40,000 yamekwishaibiwa mjini London kwa kutumia teknolojia ya keyless.

NA DAILYMAIL

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS UPATE HABARI KEMKEM ZA UCHAGUZI MKUU

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply