The House of Favourite Newspapers
gunners X

‘Magogo’ Yamponza kKigogo Mwingine – Video

0

Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya Salsabil Investment Limited, Abdulrahman Omary amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitka 15 likiwemo kosa la kusafirisha mazao ya misutu (magogo) yenye thamani ya zaidi shilingi milioni mia nne.

 

Omary amesomewa mashitaka hayo na wakili Serikali, Ladslaus Komanya mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa shau ri hilo ni la uhujumu uchumi.

 

Akimsomea hati ya mashitaka , Wakili wa Serikali Komanya amedai kuwa mshtakiwa aliyatenda makosa hayo katika maeneo tofauti ya nchi kati ya Januari 1, 2015 na Novemba 31, mwaka 2015 wakati akijua ni kosa kisheria.

 

Katika shitaka la kughushi nyaraka, Wakili Komanya amedai kuwa mshitakiwa huyo anadaiwa kughushi nyaraka ya kusafirisha mazao ya misutu kontena kumi na saba akidanganya kuwa kibali hicho kimetolewa na afisa mwenye dhamana nchini Zambia wakati akijua si kweli.

 

Leave A Reply