The House of Favourite Newspapers

MAGONJWA MAPYA YA ZINAA AMBAYO NI TISHIO

KWA SASA Magonjwa mapya huibuka kila uchao na magonjwa yaambukizwayo kwa ngono nayo ni miongoni mwao. Katika makala haya ninakuletea bakteria wanne ambao husababisha magonjwa mapya ya zinaa ambayo ni tishio la afya kwenye jamii kwa sasa.

1: NEISSERIA MENINGITIDES

Neisseria meningitidis pia hufahamika kama meningococcus, husababisha uvimbe hatari wa tando za uti wa mgongo na ubongo. Bakteria huyu amekuwa akipata umaarufu zaidi kwa kusababisha maambukizi kwenye maungo ya uzazi. Utafiti mmoja uliofanywa miaka ya 1970 ulibainisha ni kwa namna gani dume moja la sokwe lilihamisha bakteria hao hatari kutoka mdomoni na puani kwenda kwenye uume wake baada ya kujilamba sehemu zake nyeti.

Mnyama huyu (sokwe) mara kwa mara hujilamba uume wake. Takriban asilimia 10 ya watu wazima wana bakteria aina ya Neisseria katika makoo na pua zao. Tafiti zinabainisha kuwa wanaweza kuhamisha bakteria hao kupitia mabusu makali yahusishayo ndimi au kunyonya sehemu za siri za watu ambao hawana bakteria hao.

Watafiti, hata hivyo, hawana uhakika ni kwa nini bakteria hao wamesambaa kwa kasi na kuzua ugonjwa hatari kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja barani Ulaya, nchini Marekani na Canada. Hata hivyo, utafiti mmoja juu ya muwasho mkali wa mrija wa kupitisha mkojo kutoka kweye kibofu unaosababishwa na bakteria huyo ulibainisha kuwa wanaume waliopata maambukizi hayo kupitia ngono ihusishayo mdomo. Wanasayansi wanaamini kuwa, maambukizi makali ya bakteria huyo yaliyokumba kwa

na ugumba, kuharibika kwa mimba, kuzaliwa watoto njiti na hata kufariki dunia kwa watoto tumboni kwa mama. Ijapokuwa kondomu inaweza kuzuia maambukizi yake, watafiti wanatoa tahadhari juu ya usugu wa bakteria huyo kutibika na dawa za antibaotiki za azithromycin na doxycycline.

2: SHIGELLA FLEXNERI

Shigella flexneri husababisha maumivu makali ya tumbo na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao. Shigellosis husababishwa kwa kugusa moja kwa moja au kwa njia moja au nyengine kinyesi cha binadamu. Maambukizi ya bakteria huyu husababisha maumivu makali ya tumbo na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao.

Japokuwa ugonjwa huo umekuwa ukionekana zaidi kwa watoto na wasafiri kwenye nchi zenye uchumi mdogo na wa kati, watafiti walianza kupokea kesi za ugonjwa huo kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja tangu miaka ya 1970. Ugonjwa huo, wanasayansi wanaamini, umechukua njia mpya ya maamukizi kwa kutumia ngono ya kinyume na maumbile na ngono inayohusanisha midomo na kusabisha maambukizi kadhaa ya gonjwa hilo la zinaa kwa miongo minne sasa.

3: LYMPHOGRANULOMA VENEREUM (LGV)

Magonjwa mengi ya zinaa yanaweza kuepukwa kwa kutumia kondomu. LGV, mwanzo hutokea kama kipele au lengelenge kisha kushambulia mfumo wa kinga ya mwili na hivyo kusababisha uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Ugonjwa huu pia husababisha maambukizi katika njia ya haja kubwa na pia kusababisha maumivu makali ya tumbo. Katika miaka 10 iliyopita, kumekuwa na maambukizi makubwa ya LGV barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini hususani kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja. Kutumia kondomu kunaweza kupunguza uwezekano wa maambukizi na kutibu ugonjwa huu kunahitaji walau matibabu ya wiki tatu na kunywa antibaotiki kama doxycycline.

nguvu miji kadhaa ya Marekani mwaka 2015 yalichochewa na vinasaba vya karibu vya bakteria wa familia moja na Neisseria gonorrhoeae ambaye husababisha ugonjwa mwingine wa zinaa wa kisonono. Ukaribu wa bakteria hawa ulisababisha kusambaa kwa haraka kwa maambukizi hayo hatari. Kuna aina tano ya bakteria hatari wa Neisseria meningitidis duniani, lakini kwa bahati nzuri kuna chanjo za aina mbili ambazo zinapatikana na zinakinga dhidi ya aina zote za bakteria hao.

4: MYCOPLASMA GENITALIUM

Mycoplasma genitalium ni hatari sana kwa mfumo wa uzazi kwa wanawake. Mycoplasma genitalium, moja ya bakteria wadogo zaidi wanaofahamika, wanapata umaarufu mkubwa zaidi ya maumbo yao kwa kusababisha maambukizi hatari ya ugonjwa wa zinaa. Bakteria huyo aligunduliwa miaka ya 1980 na leo hii anaambukiza asilimia moja hadi mbili ya watu hususani vijana.

Maambukizi ya Mycoplasma genitalium ambayo kwa kawaida hayana dalili, wakati mwingine hufanana na dalili za kisonono na kaswende kwa kuwashwa mfululizo kwa mrija wa mkojo kwa wanaume na mlango wa kizazi kwa wanawake. Kutokana na kuweza kusamabisha maumivu makali ya nyonga kwa wanawake, bakteria huyo anahusishwa pia

Comments are closed.