Magori: Wasauz Wanaigombania Simba

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori

IMEBAINIKA kuwa wakati Simba ikitarajiwa kuondoka kwenda Afrika Kusini kuweka kambi Jumatatu ijayo, klabu kibao za Sauz zimeomba kucheza mechi za kirafiki na Simba itakapokuwa huko.

 

Msimu uliopita, Simba ilifanya vyema kwenye michuano ya kimataifa na hata kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ndiyo maana timu nyingi zimevutika kujipima na Simba.

 

Simba itaanza kambi yake huko Sauz kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo michuano yote hiyo itaanza Agosti, mwaka huu.

Awali, Simba ilipanga kuweka kambi yake nchini Marekani lakini ilibadili mipango kutokana na hali ya hewa ya joto na kuhamia kwenye baridi ambako ni Sauz.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amethibitisha kuwa klabu nyingi za Sauz zinaomba kucheza mechi na Simba itakapokuwa huko.

Magori alisema kuwa wanasubiri wakifika kule ndipo watafanya maamuzi kuona ni klabu gani ambazo watadili nazo.

 

“Tunaenda kuweka kambi Sauz lakini pia tuna mpango wa kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujipima lakini mpaka sasa sijui tutacheza na timu ipi, sababu klabu tu kubwa za pale Sauz kila mmoja anataka kucheza mechi na sisi lakini hatujui mpaka sasa tutacheza na yupi.

 

“Lakini tukikaa na kutulia wakati tunaendelea na maandalizi huku, ndipo tutafanya maamuzi na kufahamu tutacheza na timu ipi, ila ufahamu tu kila timu inataka kujipima na Simba kutokana na hatua ambayo tulipiga kwenye msimu uliopita kimataifa,” alisema Magori. Hii itakuwa mara ya pili kwa Simba kuwahi kuweka kambi yake Afrika Kusini.

UCHAMBUZI: BAADA YA MATOKEO YA KIDATO CHA 6 KUONGEZEKA, HII NDIO SIRI.. | GLOBAL RADIO


Loading...

Toa comment