The House of Favourite Newspapers

Magufuli afunika ngoma ya Kimasai

0

magufuli (3)-001Richard Bukos

MGOMBEA urais wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli ameonesha ufundi wa hali ya juu kwa kucheza ngoma ya kimasai maarufu kwa jina la Osingilio.

Magufuli alionesha ufundi huo juzi Jumanne alipokuwa amekwenda kufanya kampeni katika  wilaya Monduli, mkaoani Arusha, ambako ni ngome ya mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Mara baada ya kufika Monduli, Magufuli alipokelewa na wazee wa Monduli ambao walimtawaza kuwa Laigwenan (chifu wa kabila la Wamasai) ndipo mgombea huyo alipojichanganya katikati ya wananchi waliokuwa wakicheza ngoma hiyo kisha kuanza kuonesha ujuzi wa kuruka juu kama matakwa ya ngoma hiyo.

Wakati akiruka, wananchi wa eneo hilo walishangilia na wakidai amewafunika hata wale wazawa wanaoicheza ngoma hiyo mara kwa mara.

Baaada ya kuvishwa vazi maalum la uchifu, Magufuli alikwenda kuzuru kaburi la Hayati Edward Moringe Sokoine akiwa na Mgombea Ubunge wa  Jimbo la Monduli, Namelok Sokoine kisha kufanya mkutano mkubwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao ulifurika maelfu ya Watanzania waliofurika kusikiliza sera na Ilani ya CCM.

Leave A Reply